Author: arushatv

Na Dorin Mwanza Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea na jitihada za kuelimisha jamii ikiwa ni pamoja na kutembelea Ofisi za Vyama katika kila Mkoa na kuelezea juu ya umuhimu wa uhifadhi na utunzaji wa rasilimali za Taifa pamoja na fursa zitokanazo na Sekta ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kukuza uchumi kwa wananchi. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa uliofanyika leo jijini Mwanza. “Moja ya maelekezo tuliyoyapata kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa ni wahifadhi kushuka kwenda kila mkoa…

Read More

Katika Mkutano wa Adhara Soko kuu la Arusha Kada wa chama chamapinduzi Ccm Noel Ole Varoya amekiama chama chake hicho na kujiunga na Chadema uku akisema amechoka kua utumwani. Akimpokea kada uyo mpya wa Chadema Mwenyeliti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema amemlaribisha Noel nakumtaka kuacha tabia ya kusaliti chama chake cha Chadema. Tazama Matukio katika picha . Mwisho .

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Baada ya kuonja joto la kukosekana kwa usafiri kwa siku ya jana  kwa mgomo wa Dala Dala kwa siku nzima Jijini Arusha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra)Mkoa wa Arusha imetangaza kumaliza mgomo kwa madereva wa daladala uliodumu kwa siku moja baada ya kukubaliana na viongozi wa daladala jijini Arusha na kuahidi kutatua changamoto za bajaji zinazolalamikiwa kufanyakazi kinyume cha sheria za usafirishaji Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, ofisa mwandamizi wa LATRA mkoani Arusha , Amani Mwakalebela alisema ofisi yake imeahidi hadi tarehe 10 mwezi huu kushughulikia kero za daladala zinazotokana na bajaji…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wakazi wa Jiji la Arusha  wameonjañ joto la jiwe mara baada ya madereva wa dala dala kugoma kwa kile wanacho dai kuingiliwa na bajaji kusafirisha abiria katikati ya jiji la Arusha . Adha ya usafiri imesababishwa na mgomo wa daladala unaoendelea katika barabara zote za Jiji la Arusha na Arumeru kushinikiza kuondolewa kwa bajaji katika ruti zao. Wakazi wa Jiji la Arusha wakiwa wanasubiria usafiri wa Guta kuelekea katika maeneo ya makazi . Akizungumzia hali hiyo miongoni mwa abiria, Amina Hassan amesema mgomo huo umeanza leo asubuhi umesababisha mateso makubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha…

Read More

Na Geofrey Stephen .MONDULI JUMLA ya MIRADI 14 yenye thamani ya sh, bilioni 1.8 wilayani Monduli Mkoani Arusha, imezinduliwa ,kuwekwa mawe ya msingi ,kutembelewa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ukiwemo mradi wa maji wa sh,milioni 500.7 katika kata ya Meserani. Mkuu wa wilaya ya Monduli,Joshua Nasari alieleza hayo wakati akikabidhiwa mwenge wa uhuru katika eneo la Meserani ,ukitokea jijini Arusha, ambapo alisema kuwa miradi hiyo inatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu,Halmashauri na nguvu za wananchi. Alifafanua kuwa miongoni mwa fedha hizo kiasi cha sh,bilioni 1.17 ni kutoka serikali kuu sh,milioni 30 kutoka halmashauri na nguvu za wananchi sh,milioni…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewataka Walimu kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wanafunzi na kuwafundisha kwa weledi mkubwa, ili kulisaidia taifa kupata Wataalam wakutosha katika nyanja za Uhandisi, Sayansi na Teknolojia. Prof. Mdoe ametoa rai hiyo, wakati akifunga Mafunzo ya Walimu wa Sayansi na Hisabati mkoani Arusha, ambapo amesema serikali inahitaji kujenga na kuimarisha uchumi imara, na katika kutekeleza mradi wa SEQUIP, inatarajia matokeo chanya kutoka kwa walimu hao, baada ya kuwapatia mafunzo ya kuongeza ujuzi na umahiri katika ufundishaji na Ujifunzaji. “Lengo la mafunzo kwenye mradi wetu…

Read More