Author: arushatv

Na Mwandishi wa A24Tv Kilimanjaro . Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) awataka Maafisa Biashara wote nchini kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria. Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo. Dkt. Kijaji amesema ni jukumu la Maafisa Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua. Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa…

Read More

Na John Mhala,Longido Zaidi ya shilingi milioni 30 zimechangwa na Shirika la Mipango na Maendeleo ya Jamii Longido {CBO} na Shirika Mwenza la Nchini Marekani la Friends For African Development {FAD} kwa kushirikiana na wananchi na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Dkt Steven Kiruswa Katika kuhakikisha mtoto wa kike wa jamii ya kifugaji anapata elimu ya uhakika na huduma kadhaa za kijamii. Hayo yalisemwa na  Dkt Kiruswa katika Kitongoji cha Kaale, kijiji cha Iloirienito kata ya Iloirienito Wilayani humo mara baada ya kushiriki tukio la nguvu kazi na wananchi baada ya kuona juhudi  za wananchi katika kuisaidia serikali ujenzi…

Read More

Na John Mhala,Longido Bibi Monica Nduyai{100} Mzaliwa wa Kijiji cha Idendui Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha amesherekea siku yake ya kuzaliwa{Happy Barthday} kwa kutimiza miaka mia moja{Karne Moja} kwa kugawa msaada wa Mahindi tani 20 kwa watu wenye kuishi katika mazingira magumu {masikini} katika kata zote zilizopo katika wilaya ya Longido Mkoani Arusha. Nduyai ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Longido na Naibu Waziri wa Madini,Dkt Stephen Kiruswa alisherehekea siku hiyo nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngosuak kata ya Engarenaibor Wilayani Longido sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} na Jumuiya zake ngazi ya wilaya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .TANGA – Waumini wa dini ya Kiislamu kote  dunuani  wameaswa kujenga mazoea ya kusoma na kuchambua matukio ya tareekh ili kuweza kujua historia ya Dini yao ya vizazi  vyake. Hayo yameelezwa leo Mkoani Tanga na Mudir wa Muasas Sheikh Shaffi Muhammed Nina wakati wa maandamano ya Maombolezi ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhamad ( S.A.W ) Imam Hussein ( A.S) aliyefariki mwaka wa sitini na moja Hijiria. Sheikh Shaffi amesema  kuna haja ya kusoma na kuchambua tareekh kwa kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu vilikuja  vikiwa salama lakini kulingana na siasa za…

Read More

Na Richard Mrusha AFISA ustawi wa jamii manispaa ya Ubungo jijini Dar Naamini Nguve, amewataka wanandoa nchini wajitahidi kumaliza migogoro yao ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani. Nguve amesema kuwa katika kituo cha mabasi maarufu Magufuli kilichopo manispaa ya Ubungo jijini hapa wamekuwa wakipokea makundi ya watoto chini ya miaka 18, vijana, wazee pamoja na walemavu kutoka katika Mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuja kusaka ajira. Afisa Ustawi wa jamii manispaa ya Ubungo, Nguve, akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake. Afisa huyo wa ustawi wa jamii amesema kuwa hatua hiyo wamebaini baada ya watoto hao kufika…

Read More