Author: arushatv

Na Mwandishi wa A24tv . M’bunge wa Monduli Frederick Lowassa ameahidi kuachia ubunge wake endapo utatuzi wa mgogoro wa Shamba la Manyara ranch aliyoanzisha baba yake Edward Lowassa haitafika mwisho wa mwaka huu na wananchi kunufaika nao. Fred ameyasema hayo  April 21, 2024 katika shule ya Msingi Laiboni iliyoko kitongoji cha Esmit alipotembelea kwenye ziara ya kutembelea miradi na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM sambamba na kuzungumza na Wananchi wake kujua matatizo mbalimbali Ili kuyafikisha bungeni. Fred amesema kuwa mgogoro huo ulioanza zaidi ya miaka 26 sasa, kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei vilivyoko kata ya Esilalei…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Maliasili na Utalii inatarajiwa kesho tarehe 22.04. 2024 kutangaza rasmi matokeo ya sensa ya wanyamapori, Pamoja na kuzindua ripoti ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea nchini kwa mwaka 2023. Utangazaji na uzinduzi huu huo utajumuisha wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii utafanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha, ambapo Waziri wa maliasili na utalii Angellah Kairuki ndiye anayetarajiwa kutangaza matokeo hayo ya sensa na kuzindua ripoti hiyo. Katika mkutano wake na wanahabari jijini Arusha, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Edward Kohi ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Kusikilizwa na kufanyiwa kazi kwa asilimia 97 ya mashauri yaliyowasilishwa kwenye Baraza la Ushindani nchini (FCT) kumechochea na kuongeza uwajibikaji kwa mamlaka za udhibiti wa huduma na biashara nchini katika kusimamia ushindani wa haki. Hayo yamesemwa Aprili, 19, 2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Abbas Rugwa wakati akifungua semina ya siku moja ya utoaji wa elimu kwa wadau kuhusu shughuli za Baraza hilo. Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na wezeshi ya ushindani wa haki katika biashara na utoaji huduma na kuzitaka mamlaka za udhibiti kutekeleza azma…

Read More

Na Mosses Mashala Zanzibar . Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa Wanawake na kuwashirikisha katika ngazi ya maamuzi  na kuendeleza maendeleo nchini. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji Wanawake kiuchumi kwa Zanzibar kupitia program ya Mwanamke Shujaa ilioandaliwa na kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kushirikiana na Oryx Gas Tanzania, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Wakala wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) katika viwanja vya Maisara , Mkoa wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Serikali za Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya kero 15 zilizokuwepo awali ili kurahisisha michakato ya biashara ya nchi hizo kutegemeana kibiashara. Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban wakati wa kikao cha pamoja cha Mawaziri wa nchi zote mbili katika sekta hiyo. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban (kulia) akiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambia Mhe. Chipoka Mulenga (kulia) pamoja ma wajumbe wa Mkutano huo wa pande zote mbili wakipitia Hati ya Tamko la…

Read More

Na Mosses Mashala Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kwa jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi kutaongeza ari na kasi ya utoaji wa huduma za Uhamiaji katika Mkoa huo na Manispaa zake zote tatu . Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 19 Aprili 2024 ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema juhudi za Serikali zote mbili ni kubwa kuhakikisha Watanzania na Wageni wanaoitembelea nchini wanapata huduma zilizo…

Read More

Na Bahati Hai, Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Amiri Mkalipa,amawataka Wananchi Wilayani humo kuitunza miti waliyoipanda hadi ikue na kufikia lengo la utunzaji wa mazingira Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo na taarifa nyingi kwamba miti mingi iliyopandwa sehemu mbali mbali inakuwa ni kazi bure kwani ukosa uangalizi na hatimae miti kushindwa kukua. Akizungumza Mara baada ya kupanda miti zoezi lililoandaliwa na taasisi isiyo ya kisherikali ya Floresta katika Kijijii cha Mkombozi Wilayani humo ikiwa ni sambamba na maazimisho ya miaka 60 ya Muungano,ametaka miti hiyo kutunzwa na atakayebainika kufanya ujuma kuing’oa Sheria itachukua mkondo wake “Sisi Wilaya…

Read More