Author: arushatv

Na Mwandishi wa A24tv . Msemaji mkuu wa taasisi ya Twariqa Tulikadiriya Jailania Tanzania Shekhe Haruna Hussein amewataka wanasheria ambao wamekwenda mahakamani kupinga suala la Uwekezaji wa Bandari hapana nchini badala yake wakutane na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ili kuweka sawa Jambo Hilo Kwa maslahi mapana ya Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha shekhe Haruna alisema kwamba kitendo Cha kwenda mahakamani ni kumdhalilisha Amiri Jeshi Mkuu. “Kila Mwanasiasa ana haki ya kutoa maoni yake lakini kwenda mahakamani sio sahihi badala yake watangulize hofu ya Mungu,na waombe kukutana na Mheshimiwa Raisi na Kwa vile ni…

Read More

Na Dorin Aloyce Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kupata hati safi katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichojadili taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/2022. Pongezi hizo amezitoa katika kikao kazi cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo Wilayani Chemba. “Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilikuwa na hoja 50 ambazo ambazo zimegawanyika katika sehemu tatu, hoja za mwaka jana 25, hoja za miaka iliyopita 25 na agizo la LAAC ambalo ni moja” ameeleza Mhe.Senyamule Aidha, amesema kati ya hoja…

Read More

Na Doreen Aloyce. Serikali yatoa millioni 699 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka lenye ukubwa wa mita 20 na ambalo litapitika muda wote na kusaidia kufungua barabara Muhukuru mpaka Kizuka itakayochochea uchumi kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katka Halmashauri ya wilaya ya Songea leo tarehe 13/07/2023. “Barabara hii ni barabara muhimu, ni barabara ya huduma ni barabara ya uchumi ni barabara itakayoimarisha ulinzi,” na kipekee ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .Kilimanjaro Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuber Kidumo amejikuta akichezea kichapo kikali kutoka kwa diwani mwenzake,ABUU SHAYO wakati akiendesha kikao cha kamati Ya Mipango miji na Ardhi katika manispaa hiyo. Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita mchana wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake ,ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wakiuliza maswali mbalimbali kwa mstahiki meya huyo ili kupata ufafanuzi wa masuala ambayo wanaona hayako sawa. Mmoja Ya wajumbe wa kamati hiyo Abuu Shayo ambaye ni diwani wa kata Ya mji Mpya,katika manispaa hiyo,alihoji mchanganuo wa sh,milioni 50 zilizotumika kwenye ujenzi wa madarasa…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma BAADHI ya wadau wa Mifugo na Uvuvi Tanzania wamesema bado wanakutana na changamoto za masoko ya mazao yao hasa kutoka nchi za nje kutokana na kukosa fursa mbalimbali za kimataifa hali inayowaweka mbali na wawekezaji katika sekta ya kifedha ambazo kama wakikutana nazo wanaweza kuongeza mitaji yao nakuongeza tija ya mazao yao. Wadau hayo yaliyabainisha Jijini Dodoma kwenye maandalizi ya kushiriki mkutano wa Jukwaa la chakula Afrika 2023 ambao kwa mara ya pili unafanyikia nchini Tanzania ambapo wameiomba serikali kuwakutanisha na wafanyabiashara kutoka nje za nchi kwa kuwapa kipombele cha nafasi za maonyesho ya kimataifa. “Tunachangamoto…

Read More

Na Geofrey Stephen .Arusha Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi. amesisitiza wakandarasi waliosaini miradi ya sh, bilioni 7.282 kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wapate maji kwa araka zaidi  ikiwemo kuwatua ndoo kichwani wanawake na wananchi kwa ujumla. Mhandisi Mahundi alimetoa maagizo hayo leo Jijini Arusha kwenye halfa ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini katika wilaya za Arusha . Amesema miradi hiyo ni lazima ikamilike kwa wakati na serikali inauwezo wa kutumia wazawa katika kufanikisha hatua mbalimbali za miradi ya maji hususan ya vipuri. “Tunampongeza Mh Doctar  Samia Suluhu Hassan kwa miradi…

Read More

Na Geofrey Stephen MIRERANI Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Quen Sendiga amewataka wachimbaji wadogo wa Tanzanite ,waliopo katika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro ,mkoani Manyara, kusaidia kuibua maendeleo katika mkoa huo hususani katika sekta ya elimu ili kuisaidia jamii ya kifugaji kuwapeleka watoto kusoma. Sendiga ametoa rai hiyo jana wakati alipotembelea shule ya msingi ya Saniniu Laizer yenye mchepuo wa kiingereza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,ambapo katika shule hiyo ilijengwa na mchimbaji huyo serikali imepeleka sh,milioni 69 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo Mkuu huyo wa Mkoa alisema…

Read More