Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»DC IKUNGI AWAPELEKA WATATU TAKUKURU KUKWAMISHA UJENZI KITUO CHA AFYA IRISYA.WAMALIZA MILIONI 500

    DC IKUNGI AWAPELEKA WATATU TAKUKURU KUKWAMISHA UJENZI KITUO CHA AFYA IRISYA.WAMALIZA MILIONI 500

    0
    By arushatv on November 1, 2022 Habari

    Na Mwqndishi wa A24Tv

    Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 01/11/2022 amemuelekeza mkuu wa takukuru wilaya ya Ikungi kuanza uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watumishi watatu waliokuwa wanasimamia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Irisya tarafa ya Sepuka jimbo la singida magharibi.

    Pamoja na hatua hiyo pia amemuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Mhe. Justice Lawrance kupeleka team ya uchunguzi ambayo itakuwa na lengo la kuchunguzi mienendo ya tabia za watumishi hao watatu ili pia waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi za halmashauri

    Dc Muro amesema hatua hiyo imekuja baada ya mradi huo kukwama mara mbili kumalizika uku kiasi cha shilingi milioni 500 kikiwa kimeshatumika chote pasipo mradi kukamilika hatua iliyosababisha mradi kukwama kumalizika kwa miezi mitatu zaidi.

    Dc Muro amesema walivyofika kwa nje unaweza kuona kazi imeisha ila ukiingia ndani utabaini maabara haijakamilika, vyoo vyote vya majengo yote havijakamilika, tiles za chini hazijakamilika, jengo la mochwari ndani halijakamilika, vyoo havijafungwa vyote na masinki ya kunawia mikono hayajakamilika, uku baadhi ya majengo yakiwa tayari na nyufa kitu ambacho hakiweza kufumbiwa macho

    Katika hatua ingine ya kushangaza ni kitendo cha wasimamizi wa mradi huo kuita fundi ambae alitengeneza kipande cha ngazi za kupandia jengo la mama na mtoto na kisha kutoweka uku wakijua kuna ziara ya mkuu wa wilaya na walipoulizwa iweje walete fundi siku moja kabla na kwanini fundi huyo leo hakuwepo viongozi wote walikana kumuita na kumtambua fundi huyo uku wakijua kuna kazi imefanywa kwa siku moja tu

    Dc Muro pia ametoa maagizo ya kukamilika kwa vituo vyote vya afya ambavyo vinajengwa na hela zikiwa zote zimeshatumika na kusisitiza wasimamizi wa vituo vya afya vya Iyumbu, Ntuntu na iglanson kuwa tayari kwa lolote lile

    “Wananchi hawataki kusikia malumbano yenu kwenye ujenzi wao wanataka kuona hela zilizotolewa na Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan zinatumika ipasavyo na miradi inamalizika pasipo visingizio ” ameongeza Muro.

    Mwisho .

     

    Post Views: 62
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAMA MBARONI NJOMBE KWA KUWACHOMA MOTO WATOTO WAKE
    Next Article WAKALA WA MISITU WAPANGA KUKUSANYA BILION 3.7

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.