Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»MAMA MBARONI NJOMBE KWA KUWACHOMA MOTO WATOTO WAKE

    MAMA MBARONI NJOMBE KWA KUWACHOMA MOTO WATOTO WAKE

    0
    By arushatv on November 1, 2022 Habari

    Na Emmanuel mkulu

    Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Adelina Ng’olo mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Nyombo wilayani Njombe kwa tuhuma za kuwachoma moto watoto wake wawili katika sehemu mbalimbali za miili yao kwa kile alichodai wamemdharirisha kwa kuomba chakula kwa majirani.

    Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amewataja watoto hao waliochomwa moto kuwa ni Eliud Chatanda[7] na Elina Chatanda mwenye umri wa miaka[4] ambao walikwenda kwa majirani kutafuta chochote ili mradi siku iende lakini majirani wakaanza kumsema mama huyo kuwa anashindwa kuwalea watoto wao mpaka wanakuwa ombaomba

    Kamanda Issa amesema watoto hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena baada ya kufanyiwa ukatili huo mbaya na mama yao mzazi.

    Aidha kamanda Issa anatoa wito kwa wananchi wa Njombe katika malezi ya watoto na kwamba ukatili huo hapaswi kufanyiwa binadamu yeyote hivyo ni muhimu kuachana na vitendo hivyo.

    Edward Mlowe na Makwayi Barani ni wakazi wa Njombe ambao wanasema ukatili unaofanyika mkoani Njombe unapaswa kupingwa na kila mtu kwani hakuna sababu ya kuchukua hatua ngumu za kuwachoma watoto na kuwaharibia maisha yao badala ya kuwapa adhabu ndogondogo.

    Mkoa wa Njombe umekuwa ukikumbwa na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mara kwa mara jambo linalosababisha athari za kimwili na kisaikolojia kwa watoto hao huku jamii ikitakiwa kuchukua hatua stahiki katika kupinga vitendo hivyo.

    Post Views: 132
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRIPOTI YA SENSA CHANGAMOTO MPYA YA FURSA! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article DC IKUNGI AWAPELEKA WATATU TAKUKURU KUKWAMISHA UJENZI KITUO CHA AFYA IRISYA.WAMALIZA MILIONI 500

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.