Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»TUZO ZA UBORA ZA KITAIFA 2022/2023 KUZINDULIWA RASMI LEO.

    TUZO ZA UBORA ZA KITAIFA 2022/2023 KUZINDULIWA RASMI LEO.

    0
    By arushatv on October 27, 2022 Habari

    Na Doreen Aloyce, Dodoma

    WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuwania Tuzo za Ubora za Kitaifa kwa mwaka 2022/2023 ambazo zinahusisha Sekta mbalimbali na watu binafsi wanaofanya vizuri kwenye masuala ya Ubora ambazo zitasaidia kuitangaza nchi.

    Akizungumza na Vyombo vya Habari (leo) jana Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Tuzo za tatu za Ubora za Kitaifa Mwaka 2022/2023 Kaimu katibu mkuu wizara ya uwekezaji, Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi amesema kuwa tuzo hizo zitaleta fursa ukuaji na maendeleo ya sekta ya viwanda na Biashara.

    Amesema mashindano ya Tuzo hizo ni pamoja na Tuzo kwa kampuni bora , tuzo kwa bidhaa bora , tuzo kwa huduma bora , tuzo kwa muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi na mtu mmoja aliyefanya vizuri kwenye masusla ya ubora .

    Pia amesema mashindano hayo wadau watapata fursa ya kufahamika zaidi kwenye jamii na kushiriki kwenye mashindano ya tuzo za ubora kwa jumuia ya Afrika Mashariki , mashundano ya tuzo za ubora kwa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika na kufahamika kupata masoko zaidi.

    “Serikali kupitia wizara ya uwekezaji ,viwanda na Biashara iliona umuhimu wa kuanzisha tuzo hizi na kutoa jukumu la kuziratibu kwa shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini (TPSF) Taasisi ya viwango Zanzibar , shirikisho la wenye viwanda nchini ,”

    ” Pia tumeshirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO) ,chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania , Chemba ya Biashara , viwanda na Kilimo Tanzania na mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania “amesema Mbwasi.

    Hata hivyo amewataka watanzania kuwa mabalozi wa Kuhamasisha wazalishaji wa Bidhaa na watoa huduma kushiriki mashindano ya Tuzo za ubora za mwaka 2022/2023.

    Nae Mkurugenzi mkuu wa shirika la Viwango Tanzania Daktari Athuman Ngenya akizungumzia maandalizi yalivyo mpaka amesema kuwa yanaendelea vizuri kwa kutumia warsha mbalimbali na vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii ambapo yatasaidia kuwapata washindi.

    “Katika maandalizi haya tumewapa kipaumbele akina mama wajasiliamali kuwahamasisha ili waweze kushiriki kwani ni wengi ambao wamejikita kwenye ujasiliamali.” Amesema Ngenya

    Kwa upande wake Hafsa Ali Slim Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwango ambapo akimuwakilisha Mkurugenzi ZBS
    amesema kuwa wanatarajia kutoa uelewa kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa upande wa Zanzibar ili waweze kushiriki kwa wingi zaidi.

    Mwisho.

    Post Views: 81
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTaasisi ya EBN yachimba mabwawa kusaidia wanyamapori kukabiliana na Ukame.
    Next Article MILIONI, 500 ZAKAMILISHA KITUO CHA AFYA WANACHI WAMSHUKURU RAIS SAMIA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.