Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Uncategorized»Taasisi ya EBN yachimba mabwawa kusaidia wanyamapori kukabiliana na Ukame.

    Taasisi ya EBN yachimba mabwawa kusaidia wanyamapori kukabiliana na Ukame.

    0
    By arushatv on October 27, 2022 Uncategorized

    Taasisi ya EBN yachimba mabwawa kusaidia wanyamapori kukabiliana na Ukame.

    Mwandishi wetu.

    Babati.Taasisi EBN ambayo inamiliki Kitalu Cha uwindaji katika eneo la jumuiya ya uhifadhi wa Wanyamapori ya Burunge ,imechimbwa bwawa ili kusaidia wanyamapori kupata maji.

    Uamuzi huo umefikiwa kutokana na Ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi umeanza kusababisha vifo kwa wanyamapori katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge(WMA) wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

    Burunge WMA ipo kati kati ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Taifa ya Manyara na inaundwa na vijiji 10 ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 24,319.

    Licha ya wanyamapori kuanza kufa pia kumeongezeka matukio ya ujangili na migogoro baina ya wananchi na wanyamapori kutokana na wanyamapori hao kuanza kuingia maeneo ya vijiji kusaka maji na malisho.

    Meneja Uhusiano wa EBN, Charles Sylvester alisema wameamua kuchimba mabwawa na kutoa maji kwa Wanyamapori ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani maji yamepungua sambamba na malisho.

    “Hivi Sasa eneo letu kuna idadi kubwa ya Wanyamapori tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kupewa Kitalu hiki ambapo pia Sasa Wanyamapori wamekuwa rafiki na watu na kuwezesha utalii wa picha na Makundi makubwa ya wanyamapori yamerejea katika Kitalu”alisema

    Alisema wameimarisha pia doria za kupambana na ujangili na uvamizi ndani ya hifadhi kwa kushirikiana na Mamlaka ya usimamizi Wanyamapori ( TAWA),askari wa Burunge WMA, Maafisa wanyamapori na askari wa hifadhi za Taifa ( TANAPA).

    ” Tunatumia zaidi ya milioni 400 kwa mwaka kukabiliana na ujangili na hasa kipindi hiki Cha Ukame ambapo wanyamapori wanasogea vijijini”alisema

    Katibu wa Burunge WMA,Benson Mwaise akizungumza na Mwananchi alisema Katika siku za karibuni wameanza kufa kutokana na kukosa maji na kuzama kwenye tope kutokana na ukame.

    “Hali ni mbaya sana ya Ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi tumeanza kupata kesi za wanyama kufa , wengine kuzama kwenye tope wakitafuta maji na wengine kuingia vijijini”alisema

    Mwaise alisema,wanyamapori katika vijiji 10 ambavyo vinaunda jumuiya hiyo ya uhifadhi ambayo ipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara,wameanza kuingiza mitaani kwenye nyumba za watu kunyang’anyana maji na watoto.

    Alisema wanaomba Usaidizi wa wadau kukabiliana na changamoto ikiwepo kuchimba Maji .

    Mwenyekiti mstaafu wa Serikali ya Kijiji cha Vilima vitatu,Erasto Belela alisema athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kubwa lakini Mahusiano mazuri baina ya vijiji na mwekezaji EBN imesaidia kupunguza athari.

    “Uzalishaji chakula umepungua sana lakini kupitia Utalii walau vijana zaidi 120 wameajiriwa kwa mwekezaji ,tumesaidia kujengewa shule ,kupata maji na kupata mgao wa fedha za maendeleo”alisema.

    Alisema kama sio wawekezaji hao hali ya maisha katika vijiji 10 vinavyounda WMA ya Burunge ingekuwa ngumu kiuchumi.

    Mwisho

    Post Views: 38
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMRADI MKUBWA WA BILIONI 3.2 KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA BUMBULI
    Next Article TUZO ZA UBORA ZA KITAIFA 2022/2023 KUZINDULIWA RASMI LEO.

    Related Posts

    SHEHENA LA MBOLEA ILIYO JAZWA MCHANGA YAKAMATWA WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO

    March 5, 2023

    Wadau wa Tehama mkoani Arusha watakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama.

    February 28, 2023

    KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA ASISITIZA MAFUNZO KUTOKA TUME YA USHINDANI NCHINI

    February 23, 2023

    TANESCO NCHINI KUTEKELEZA MIRADI YA UZALISHAJI UMEME, KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII

    February 23, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.