Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WIZARA YA MAJI, NISHATI NA MADINI ZANZIBAR YATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI, TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    WIZARA YA MAJI, NISHATI NA MADINI ZANZIBAR YATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI, TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    0
    By arushatv on September 30, 2022 Habari

    Na Mwanfishi wa A24Tv . Geita

    Timu ya wataalam ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Nishati na Madini, Mhandisi Said Mdungi kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar imetembelea banda la Tume ya Madini na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC)  kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita.


    Mara baada ya kupata elimu kuhusu madini mbalimbali yanayopatikana nchini pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye Sekta ya Madini wameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa usimamizi mzuri wa sekta ya madini na kuongeza kuwa wataendelea kufanya ziara mbalimbali nchini kwa ajili ya kujifunza siri ya usimamizi mzuri wa Sekta ya Madini.

    Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Mkurugenzi wa Idara ya Nishati na Madini Zanzibar, Mhandisi Said Mdungi amesema kuwa lengo la kutembelea maonesho hayo, ni kujifunza namna shughuli za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini sambamba na fursa nyingine  muhimu zilizopo nchini ili kupata uzoefu na kuboresha utendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Sekta ya Madini.

    “Ikiwa ni sehemu ya kuimarisha muungano, tutaendelea kushirikiana kupitia Sekta ya Madini kwa kubadilishana uzoefu ili tupige hatua na kuvutia wawekezaji wengi zaidi nchini Zanzibar,” amesema Mhandisi Mdungi.

    Post Views: 220
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleDC NJOMBE:KUACHA ARV NA KUKIMBILIA MITISHAMBA NI HATARI KUBWA
    Next Article AFISA MADINI MKOA WA GEITA AWATAKA WADAU WA MADINI KUJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.