Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»DC NJOMBE:KUACHA ARV NA KUKIMBILIA MITISHAMBA NI HATARI KUBWA

    DC NJOMBE:KUACHA ARV NA KUKIMBILIA MITISHAMBA NI HATARI KUBWA

    0
    By arushatv on September 30, 2022 Makala

    Na Emmanuel octavian

    Watu wanaotelekeza matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi ARV na kukimbilia kutumia dawa za asili(mitishamba)wameonywa vikali kwani kunaweza kuwasababishia madhara zaidi endapo dawa hizo hazitathibitishwa na mkemia mkuu.

    Katika mkutano na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kijiji Cha Lunguya mtwango wilayani Njombe mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema ni hatari kubwa kutelekeza dawa za ARV kisha kunywa dawa za mitishamba na kwamba jambo hilo linapaswa kupingwa kwa nguvu kubwa.

    Mganga mkuu wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe Dokta Suke Maghembe amekiri kuwapo kwa madhara juu ya kutumia dawa za asili ambazo hazijathibitishwa na kwamba watumiaji wa ARV wanapaswa kuendelea kuzitumia kwa malengo.

    Katibu wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Gehazi Mhada anasema baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wamekuwa wakikata tamaa ya kutumia dawa wakidai wamechoka jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao huku Jackson Kaduma ambay ni MVIU akisema kitendo cha kupima VVU mtu mmoja kwa majina tofauti na maeneo tofauti kunasababisha mkoa wa Njombe kuonekana kinara katika maambukizi ya vvu.

    Roida Wandelage ni diwani viti maalum ambaye anasema vikundi vingi vya WAVIU vinapaswa kusaidiwa kwa mahitaji mbalimbali huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi.Tekla Sadala akiwaonya baadhi ya watumishi wa afya wenye tabia ya kuwakaripia waviu wanaokwenda kuchukua dawa.

    Post Views: 136
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWaziri Kijaji amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.
    Next Article WIZARA YA MAJI, NISHATI NA MADINI ZANZIBAR YATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI, TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.