Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Waziri Kijaji amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.

    Waziri Kijaji amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.

    0
    By arushatv on September 30, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv Dodoma

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.)  amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.

    Dkt. Kijaji ameyasema hayo Sepetemba 26, 2022 jijini  Dodoma alipokutana na wadau wa sekta ya nguo na  walio chini ya Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania (TEGAMAT) ili kujadili changamoto wanazokutana nazo.

    Aidha, Waziri Kijaji amewashauri wadau hao kutokufunga viwanda, kwa kuwa ni sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana.

    “Njoni tukae tuongee, tupange kwa.pamoja tuone cha kufanya, tunataka viwanda vifanye kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita amnayo ni sikivu”.  Amesema Dkt. Kijaji.

    Aidha ameongeza  kuwa nia ya Serikali ni kuona viwanda nguo vya Tanzania vinakua shindani  na vinahudumia  Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Akiongea mbele ya Waziri Kijaji, Katibu Mtendaji  wa TEGAMAT Bw. Adam Zuku ameomba kuwe na ushindani wa haki na usawa kati ya waingizaji vitenge na wazalishaji ili waweze kushindana katika soko la nje

    “Tunatamani kuhudumia soko la SADC,EAC, ACFTA” alisema Zuku.

    Aidha, Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wameiomba Serikali kuanzisha mitaala ya nguo kwa kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wataalamu hao . Pia  wameiomba tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali za Serikali kujumuishwa kwa pamoja ili kuwapunguzia usumbufu na gharama kubwa za uendeshaji.

    Post Views: 166
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMWANAHABARI WA WASAFI FM ATISHIWA KUTEKWA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article DC NJOMBE:KUACHA ARV NA KUKIMBILIA MITISHAMBA NI HATARI KUBWA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.