Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA YAZINDULIWA RASMI WAKULIMA WAJITOKEZA KWA WINGI

    MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA YAZINDULIWA RASMI WAKULIMA WAJITOKEZA KWA WINGI

    0
    By arushatv on August 4, 2022 Makala

    Na Geofrey Stephen . Arusha.

    Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi yana mchango mkubwa katika upatikanaji wa malighafi za nchi,na kuweza kupata masomo ya nje huku yakisaidia kuchangia ukuaji wa uchumi kwa maendeleo ya nchi.

    Ameyasema hayo jijini Arusha ,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati akifungua maonyesho ya kilimo na mifugo nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi Njiro yenye kauli mbiu ya”agenda 10/30 kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi”.

    Alisema kuwa, maonyesho hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali endapo elimu ya kutosha itatolewa na kuenea kwa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya killimo na ufugaji wa kisasa .

    Aidha aliwataka watalaamu wa kilimo nchini kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ili walime na kufuga kisasa na kuepukana na kuondokana na zana za zamani na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao.

     

    Naye Sheikh Shafi Muhammad MemonSheikh wa Mikoa wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara Jumuiya ya Waislamu Wa Ahmadiyy alisema kuwa,maonyesho hayo yameshirikisha waonyeshaji 200 kutoka Taasisi mbalimbali licha ya taarifa kuchelewa juu ya uwepo wa maonyesho,lakini mwitikio bado ni mkubwa sana.

    Aidha aliwaomba wananchi wa mikoa ya Kanda ya kaskazini kutembelea ili kujionea mambo muhimu kwa ajili ya wakulima na wafugaji ili kuboresha kilimo na ufugaji wao ikiwemo banda la jumuhiya  hiyo ya waislamu kanda ya kazkazini kujipatia vitabu vya dini pamoja na ushauri wa maswala ya dini

    Mwisho.

    Post Views: 372
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTanzania na Zambia kuendelea kushirikiana katika kukuza kibiashara
    Next Article WAMILIKI WA MAGARI YASHULE WAONYWA UKAGUZI MAGARI YA KUBEBA WANAFUNZI

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.