Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»WAMILIKI WA MAGARI YASHULE WAONYWA UKAGUZI MAGARI YA KUBEBA WANAFUNZI

    WAMILIKI WA MAGARI YASHULE WAONYWA UKAGUZI MAGARI YA KUBEBA WANAFUNZI

    0
    By arushatv on August 4, 2022 Break News

    Na Geofrey Stephen , ARUSHA

    Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha(RTO),Solomon Mwangamilo amewaonya vikali wamiliki wa magari watakaoshindwa kuyafikisha magari yao kituoni ili yaweze kukaguliwa na kusisitiza watachukua hatua za kuwanyang’anya leseni za usafirishaji sanjari na kuwafikisha mahakamani.

    Mwangamilo ametoa kauli hiyo leo wakati akiongoza zoezi la ukaguzi wa magari ya wanafunzi ambalo limeanza leo nchi nzima na kutaraji kukamilika Agosti 13 mwaka huu.

    Katika zoezi hilo RTO,Mwamgamilo alisema kuwa wataanza kukagua magari yote ya wanafunzi katika wilaya za Arusha,Arumeru,Monduli,Karatu,Longido na kisha Ngorongoro ambapo jumla ya magari takribani 400 yanataraji kukaguliwa.

    Akiongoza zoezi la ukaguzi RTO Mwangamilo alisema kuwa endapo mmiliki yoyote wa gari la wanafunzi atakayeshindwa kulifikisha gari lake kukaguliwa atanyang’anywa leseni ya usafirishaji na kisha kufikishwa mahakamani.

    “Natoa angalizo endapo mmiliki yoyote atakayeshindwa kulifikisha gari lake likaguliwe kituoni tutamchukulia hatua kali za kisheria”alisema Mwangamilo

    Hatahivyo,alisisitiza kuwa zoezi la ukaguzi wa magari ya wanafunzi mkoani Arusha limelenga kuhakikisha magari yote yanayosafirisha wanafunzi yanakuwa katika viwango vya ubora ili kuepusha ajali za barabarani.

    Alisema kuwa katika zoezi hilo watatoa vibali maalum baada ya kujiridhisha na ubora wa gari husika na katika ukaguzi huo utahusisha kila mfumo wa ukaguzi na kutoa ushauri wa kitaalamu wa namna mmiliki wa gari atarekebisha gari lake.

    “Ukaguzi huu hautaingiliana na ratiba ya masomo ya wanafunzi hivyo wamiliki wa magari hatutarajii wawe na visingizio vya aina yoyote hili zoezi sio wito ni lazima kwa kuwa ni zoeI la nchi nzima”alisisitiza Mwangamilo.

    Mwisho.

    Post Views: 79
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA YAZINDULIWA RASMI WAKULIMA WAJITOKEZA KWA WINGI
    Next Article UTATA WAIBUKA KUHUSU UJENZI WA JENGO LA BIASHARA ARUSHA,JIJI WAPIGA “STOP”, KIGOGO CCM AHUSISHWA

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.