Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Tanzania na Zambia kuendelea kushirikiana katika kukuza kibiashara

    Tanzania na Zambia kuendelea kushirikiana katika kukuza kibiashara

    0
    By arushatv on August 4, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24tv .

    Tanzania na Zambia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kuibua fursa za biashara na kutatua mara moja changamoto zilizopo na zitakazojitokeza katika uwekezaji na biashara ili kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.

    Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Chipoka Mulenga walipokutana na kujadiliana kuhusu masuala ya uwezeshaji, biashara na kukuza uchumi baina ya Tanzania na Zambia katika kikao kilichofanyika Agosti 3, 2022, Jijini Dar es Salaam.

    Mawaziri hao walikutana kufuatia maagizo yaliyotolewa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia katika kikao chao kilichofanyika Ikulu Dar es Salaam tarehe 2 Agosti 2022 ambapo waliagiza Mawaziri wa Biashara kukutana mara moja kujadili masuala ya biashara baina ya Tanzania na Zambia.

    Dkt kijaji ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazofanyiwa kazi ni pamoja na ucheleweshaji wa kuruhusiwa magari ya Tanzania katika mpaka wa Tunduma Nakonde, Wafanyabiashara wadogo wakinyanganywa pasi zao za kusafiria, na Madereva Watanzania kuibiwa mizigo

    Kwa upande wake Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambia amesema wanafanyia kazi changamoto zilizowasilishwa huku akisisitiza lengo ni kuimarisha biashara ndani ya Afrika

    Katika kikao hicho, Mawaziri walikubaliana kufanya kikao cha pamoja ambacho kitajadili kwa kina masuala ya kibiashara na changamoto zilizopo baina ya Tanzania na Zambia. Waziri wa Zambia aliahidi ndani ya wiki mbili kuwasilisha mapendekezo ya tarehe za kikao hicho na ilikubalika kitanguliwe na kikao cha Sekta Binafsi.

    Aidha Mawaziri hao walisisitiza kuendeleza ushirikiano ambao umekuwepo tangu enzi za Mhe. Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Keneth Kaunda, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Zambia na sio kwa kushindana.

    Vilevile, Mawaziri hao walikubaliana kuendeleza dhamira nzuri ya Waheshimiwa Marais wa nchi zote mbili ya kuondoa vikwazo na kuwezesha biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi na hatimaye ajira kwa wananchi wa pande zote mbili.

    Post Views: 185
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBEI YA MAFUTA WADAU WATOA MAONI ! KUPANDA TENA MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA YAZINDULIWA RASMI WAKULIMA WAJITOKEZA KWA WINGI

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.