Author: arushatv

Na Joseph Ngilisho ARUSHA RAIS Samia suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani ,Mei Mosi yanayotarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Arusha. Akiongea na vyombo vya habari Mkoani hapa, Rais wa Shirikisho la wafanyakazi Tanzania,TUCTA, TUMAINI PETER NYAMHOKYA amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa mpira wa Sheikhe Amri Abeid siku ya Mei Mosi. Rais wa Shirikisho la wafanyakazi Tanzania,TUCTA, TUMAINI PETER NYAMHOKYA Akizungumza na Vyombo vya Habari Jijini Arusha . Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni  inayosema,”Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha” inaakisi uhalisia…

Read More

Na. Beatus Maganja Wananchi walioathiriwa na mafuriko wilayani Rufiji wameiona thamani na umuhimu wa uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA baada ya leo Aprili 16, 2024 kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa taasisi hiyo yenye thamani ya shillingi millioni 20 ikiwemo tani 6.4 za unga wa sembe, Kilo 666 za maharage na magodoro 186. Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA akimkabidhi misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge, Kamishna Msaidizi mwandamizi Abraham Jullu amesema TAWA imeguswa na janga la mafuriko lililowapata majirani na wadau namba moja wa uhifadhi wananchi wa Rufiji ambao…

Read More

Na mwandishi wa A24tv. Kwa ufupi:Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro, mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuangukia kwenye mtaro wa kupitisha maji Siha.Mtu mmoja amefariki dunia Kijijii cha Muwara Wilaya Siha, Mkoani Kilimanjaro kwa kuangukia kwenye mtaro uliojaa maji na kushindwa kujiokoa akitoka matembezini kurejea nyumbani nyakati za usiku Diwani wa kata ya Makiwaru Wilayani humo Ezekiel Lukumay Akizungumza na Mwananchi Digital amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Wilsoni Mollel(56) mkazi wa kijiji cha hicho ambaye alifariki dunia April 13, mwaka huu wakati akirudi nyumbani kutoka matembezi ambapo wasamaria wema waliukuta mwili njiani na kutoa…

Read More

Na Lilian Kasenene, Morogoro Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeeleza kuwa inatamani kuwa na maghala makubwa ya kuhifadhi malisho katika kila Halmashauri ili kuepuka changamoto ya ukosefu wa chakula kipindi Cha ukame. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia mifugo Profesa Daniel Mushi alisema hayo mjini Morogoro katika siku ya Malisho na Kongamano la Kisayansi la Nyanda za Malisho Tanzania linaloendelea. Alisema kama kila Halmashauri itatenga na kujenga maghala ya Malisho kama ilivyo kwa Wizara ya Kilimo ambayo ina maeneo mengi yenye maghala ya kuhifadhi mazao mfano mahindi, ni Imani yake kuwa suala la mifugo kufa kwa wingi kipindi Cha…

Read More

Na Mwandisbi wa A24tv. Kaya zaidi ya 40 hazina mahali pakulala baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji katika Kijiji cha Wiri, Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro. Siha.Kaya zaidi 40 zimezingira na maji katika Kijiji cha Wiri, kata ya Gararagua, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo na kusababisha mafuriko. Akizungumza na Mwananchi digital kwa njia ya simu Leo, April 14, 2024 Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Christopher Timbuka, amethibitisha kutokea kwa maafa hayo na kuwataka wananchi waliopo maeneo hayo kuondoka na kutafuta sehemu salama za hifadhi. Amesema pamoja na wananchi kuzingirwa na maji, pia miundo…

Read More

Na. Beatus Maganja Timu ya Maofisa uelimishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imeweka kambi maalumu wilayani Rufiji yenye lengo la kutoa elimu ya namna ya kuepuka madhara yatokanayo na mamba na viboko kwa wananchi walioathiriwa na mafuriko wilayani humo. Hayo yamesemwa leo na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wilayani humo. “TAWA tumeweka Kambi katika wilaya ya Rufiji kufuatia mafuriko yaliyojitokeza katika wilaya hii yaliyoathiri watanzania wenzetu” amesema. “Jambo lililotuleta hapa, kwanza ni kutoa pole kwa watanzania wenzetu ambao wamekumbwa na mafuriko haya, lakini pia tumekuja mahsusi kwa ajili ya…

Read More