Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WATOTO WA KIKE ZAIDI YA 7000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHAJI UJUZI

    WATOTO WA KIKE ZAIDI YA 7000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHAJI UJUZI

    0
    By arushatv on November 18, 2022 Habari

    KIASI cha shilingi bilioni 45 kinatarajia kuwanufaisha watoto wa kike na wanawake zaidi ya 7000 kutoka wilaya 12  nchini Tanzania kupitia  mradi wa uwezeshaji na ujuzi (ESP)  programu ya miaka 7 (2021-2028)

    Mradi huo unatekelezwa na Muungano wa vyuo na Taasisi za ufundi Canada (CICan) kwa  ushirikiano wa karibu na wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Tanzania (MOEST)kupitia idara ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (DTVET)unaofadhiliwa na serikali ya Canada.

    Akizungumza na waandishi wa  habari jijini Arusha leo katika warsha ya siku nne ya muelekeo wa  ubia kwa ajili ya mpango huo,Mshauri wa mradi wa uwezeshaji kupitia ujuzi (ESP) ,Dokta Alice Mumbi amesema kuwa,mradi huo utaimarisha njia mbadala za elimu,Ajira,kijiajiri na ujasiriamali  kwa wanawake na wasichana .

    Dokta  Mumbi amesema kuwa,mradi huo utafanya kazi na vyuo vya maendeleo  ya wananchi  (FDCs ) na asasi za kijamii (CBOs) katika jamii 12 nchini Tanzania ,na unalenga kuongeza viwango vya  ushiriki kati ya wanawake na wasichana katika programu  za mafunzo ya ujuzi na kuboresha upatikanaji wa mafunzo ya biashara ,ujuzi,jinsia na haki za binadamu katika jamii zao.

    Aidha amesema kuwa,mradi huo utapanua  fursa katika sekta rasmi na zisizo rasmi kupitia usaidizi  baada ya mafunzo ili kuingia kwenye ajira au kujiajiri.

    Aidha amesema kuwa mradi huo utafanya kazi na vyuo vya maendeleo ya wananchi 12 vilivyochaguliwa pamoja na asasi za kijamii 12 zilizochanguliwa kwa kuanzisha mtandao wa timu za jinsia na washauri wa kike,kushirikisha jamii katika shughuli za kukuza uelewa wa kijinsia juu ya faida za elimu kwa wanawake na uwezeshaji wa kiuchumi na kutoa mafunzo endelevu kwa washirika hao ya kujenga uwezo katika usawa wa kijinsia ,haki za binadamu,mbinu za ufundishaji na mafunzo ya watu wazima.

    Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya elimu,sayansi na teknolojia,Francis Michael  amesema  kuwa wizara hiyo ni wizara muhimu katika utekelezaji  wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi  ya wanawake na watoto nchini Tanzania hasa kwa kuwawezesha wanawake kufuata fursa za kiuchumi na kijamii,kuendeleza mazingira wazushi kwa mahusiano ya usawa wa kijinsia na kwa kusaidia nafasi salama kwa wanawake katika jumuiya zao.

    Naye Mkuu wa uendeshaji na Mshauri (maendeleo )masuala ya kimataifa Canada amesema kuwa,Bronwyn Cruden  Canada inajivunia  kuunga mkono ukuaji wa mpango mpya wa mwitikio wa kijinsia nchini Tanzania kupitia mpango wa uwezeshaji kupitia ujuzi.

    Amesema kuwa, ESP inatoa fursa kwa Canada kuendeleza uwekezaji wake mwingine katika maeneo ya utekelezaji ya elimu,usawa wa  kijinsia, haki  za binadamu,na ukuaji wa uchumi ambao unafanya kazi kwa kika mtu.

    “Canada imekuwa mshirika  wa  muda  mrefu katika sekta ya elimu ya Tanzania ,msaada baina ya  nchi mbili kimsingi unalenga katika kuboresha ubora na umuhimu wa ufundishaji katika shule za msingi,sekondari, na vituo vya mafunzo ya ufundi na ufundi hasa ujuzi na elimu na mafunzo ya ufundi na ufundi (TVET) ni muhimu  katika kupunguza ukosefu wa  ajira,ukosefu wa usawa na umaskini na kukuza ukuaji wa uchumi na maendeleo”amesema .

    Kwa upande wake Makamu wa Rais ,kimataifa ,vyuo na Taasisi Canada  ,Alain Roy  amesema kuwa,vyuo na taasisi  Canada inajivunia  kupewa  fursa na wizara ya elimu, sayansi na Teknolojia na masuala  ya kimataifa ya Canada kufanya programu  hiyo kwa washirika wa FDCs na AZAKIs .

    Post Views: 97
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleLATRA ARUSHA SASA NI LESENI ZA MAGARI MAKUBWA YA ABIRIA WAMILIKI WAJIPANGE
    Next Article NI HATARI NA TISHIO DAWA ZA KUKUZA MIFUGO WANANCHI HATARINI !

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.