Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Health»WAJAWAZITO WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI.

    WAJAWAZITO WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI.

    0
    By arushatv on November 23, 2022 Health

    Na Mwandishi wa A24Tv

    Wajawazito wametakiwa kuzingatia lishe bora inayoambatana na kufanya mazoezi wakati wote wa ujauzito ilibkulinda Afya ya mama na Mtoto.

    Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Tameke Joketi Mwegelo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mtendaji wa kata ya Charambe Theodora Malata katika hafla ya kuelekea uzinduzi wa Temeke Maternal Jogging uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Zakhem wilayani Temeke ,Dar es Salaam ukiwa na lengo la kuihamasisha jamii kuhusiana na lishe bora wakati na baada ya ujauzito utakaosaidia kujenga kizazi bora.

    DC Joketi kupitia kwa muwakilishi wake Theodora ameishukuru Kampuni ya Hatua Group Afrika inayoratibu program ya BUSELA kwa kuwapatia vifaa vinavyotumika wakati wa Kujifungua ” Delivery Kits” Mia mbili kwa Wajawazito zaidi ya Mia mbili huku akitoa wito Kwa wajawazito hao kuzingatia lishe bora na kuzingatia mazoezi hata baada ya kujifungua.

    Programu ya BUSELA imekuwa ikitoa elimu ya Afya ya Uzazi,lishe Bora, mazoezi na kuwajenga kisaikolojia Wajawazito kabla na baada ya kujifungua lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi huku mpango huo ukiwa ni wa miaka mitano utakaofanyika mikoa yote nchini,uzinduzi rasmi wa Maternal Jogging utafanyika february 2023.

    Post Views: 82
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBASHIRU AWAVURUGA VIGOGO WA CCM ! CHADEMA YASUSIA UCHAGUZI 2024-2025 MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article NABII MKUU GEORDAVIE AGAWA MISAADA NCHINI BURUNDI APEWA TUZO YA HESHMA

    Related Posts

    MIAKA 5, YA MREMBO MASIPETII MSICHANA MDOGO ALIYEJITOLEA KUSAIDIA JAMII NA KUACHA KAZI, ANAMILIKI NYUMBA YA MILLION 280

    March 11, 2023

    DKT MOLLEL ATOA MAJIBU MALALAMIKO UBOVU WA CHF.

    February 23, 2023

    APOTEZA MAISHA KWA KUCHAPWA FIMBO 70 ZA KIMASAI ! KOSA LA KUMTUKANA MAMA YAKE MZAZI MATUSI YA NGUONI

    January 10, 2023

    DC RUNYANGO VIJANA MJITAMBUE KATIKA AFYA NDIO MAISHA ,MJIKINGE NA MAAMBUKIZI

    December 12, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.