Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Siasa»UWT NJOMBE WATAKIWA KUVUNJA MAKUNDI

    UWT NJOMBE WATAKIWA KUVUNJA MAKUNDI

    0
    By arushatv on November 17, 2022 Siasa

    Na Mwandishi wa A24Tv Njombe

    Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter ameagiza kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwapo katika jumuiya ya wanawake UWT mkoa wa Njombe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi ndani ya chama hicho na kwamba hivi sasa kinachotakiwa ni kuungana kufanyakazi.

    Katibu huyo ametoa agizo hilo baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo ngazi ya mkoa uliomchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wa UWT pamoja na wajumbe mbalimbali huku akisema anataka kuona kazi zinakwenda na sio kuendekeza makundi.

    Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Esteria Mbwilo,Tumain Mtewa na Neema Mbanga wamesema wanamatumaini makubwa toka kwa Viongozi wao katika kuhakikisha maendeleo yanasonga

    Msimamizi wa uchaguzi huo Juma Sweda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Makete amesema Wajumbe hao wamemchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wao kwa kumpa zaidi ya kura 200.

    Baada ya Kutangazwa mshindi katika nafasi ya uenyekiti wa UWT mkoa Bi.Kevela ameahidi kwenda kutekeleza yale wanawake waliyomtuma ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi wa wanawake.

    Post Views: 120
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBISKUTI ZA BANGI TISHIO JIPYA KWA WANAFUNZI WA VYUO ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV .
    Next Article Serikali Kutengeneza Mfumo wa Kielotroniki kubaini wasio fanya Kazi Maafisa Ogani .

    Related Posts

    MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

    March 5, 2023

    CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

    January 17, 2023

    JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

    January 4, 2023

    MIKUTANO YA HADHARA RUKSA IGP WAPE VIBALI MUDA WOWOTE

    January 3, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.