Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Elimu»MKUU WA WILAYA MAKTABA SASA ZIWE KATIKA MFUMO WA KIMTANDAO KWENDANA NA KASI YA TEKNOLOJIA

    MKUU WA WILAYA MAKTABA SASA ZIWE KATIKA MFUMO WA KIMTANDAO KWENDANA NA KASI YA TEKNOLOJIA

    0
    By arushatv on November 8, 2022 Elimu

    Na Geofrey Stephen  Arusha

    MKUU wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amewataka watunzi wa vitabu  vya elimu hapa nchini ,kuanza mabadiliko ya kuingiza machapisho ya vitabu  kwenye  mfumo wa maktaba mtandao ili kuwafikia wasomaji  waliowengi kupata taarifa kwa gharama  nafuu
    Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizindua mfumo  wa usomaji wa vitabu mtandaoni katika chuo cha uhasibu Arusha (IAA)  unaoratibiwa na shirikisho la Maktaba za vyuo vikuu na taasisi zilizofanya utafiti COTUL.
    Alisema kwa sasa dunia  imeingia kwenye mabadiliko ya kimfumo na hivyo vitabu vyote vinavyochapishwa hapa nchini vinapaswa kuingizwa kwenye mfumo wa kisayansi na teknolojia katika kutoa huduma kisasa.
    “Tunataka vitabu vyote vinavyotungwa na watunzi wetu hapa nchini wakiwemo maprofesa vionekane kwenye Mtandao ili elimu yetu hapa nchini iweze kusomeka kwenye mfumo wa kidunia”
    Naye kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha,dkt Cairo Mwaitete alisema kuwa mfumo wa kuingiza machapisho kwenye mtandao kutapunguza gharama za kupata taarifa hususani kwa wanafunzi waliopo nje ya nchi

    Alisema mabadiliko hayo yatakwenda kupanua wigo kwa wasomaji kupata taarifa za ndani wakiwa nje ya nchi na kuongeza ushindani wa elimu duniani. 

    “Kupitia Cotul kutasaidia watanzania wote kuwa  na uwezo wa kupata taarifa kwa gharama nafuu,tunaomba wizara ya elimu iwezeshe miundo mbinu  ili gharama za uchapishaji ziwe nafuu”
    Kwa upande wake Mkurugenzi  mkuu wa bodi ya huduma za maktaba, dkt. Mboni Amiri alisema kwa sasa bodi ya huduma za maktaba ipo katika hatua ya kuhama kutoka maktaba za kawaida na kuingia kwenye mfumo wa kielekitroniki. 

    “Kwa sasa tupo mbioni kutengeneza sera ya kitaifa ya huduma za maktaba nchini ambayo haikuwepo ili kusimamia haki za machapisho ya watunzi”

    Naye mwenyekiti wa Cotul,Sydney Msonde alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo ni kutokana na mabadiliko  ya kidunia kutoka analogi na kwenda kidigtal.

     

    Alisema matarajio ni kuona machapisho ya kisayansi ya watafiti yanaweza kufundishwa kwa mfumo wa kielekitroniki na kuwafikia wasomi wengi zaidi duniani.

     

    Awali profesa Alfred  Sife, makamu mkuu wa chuo cha ushirika Moshi alizitaka maktaba zote hapa nchini kuboresha huduma zake  ili ziendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kupanua wigo wa kutoa huduma duniani .

    Wageni waliofika katika uzinduzi huo wakifatilia mjadala kwa umakini .

     

     

     

     

    Post Views: 128
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSITA WAFARIKI DUNIA MUME NA MKE KWA AJALI YA GARI KITETO
    Next Article VIKOSI KASI 3 KUCHUNGUZA AJALI YA NDEGE BUKOBA MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV

    Related Posts

    SHULE YA BILIONEA SANINIU LAIZER YAPATA UFADHILI MZITO WA MADAWATI NA MEZA ZA KISASA

    March 13, 2023

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri.mkubwa

    February 28, 2023

    WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI WALIO FUTIWA MATOKEO YA MITHIANI WA KIDATO CHA NNE

    February 9, 2023

    WANAFUNZI 170 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KUTOKA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI.

    January 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.