Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Maganya aitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.

    Maganya aitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.

    0
    By arushatv on November 28, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen .Arusha
    Arusha.Mwenyekiti wa wazazi Taifa (MCC) Fadhili Maganya ameitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika maswala mbalimbali ya maendeleo anayoendelea kuyafanya .
    Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akikaribishwa rasmi na jumuiya ya wazazi mkoani Arusha

    Maganya amesema kuwa, Rais Samia amekuwa akifanya mambo mengi sana ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuyaunga mkono na kuhakikisha kazi inasonga mbele.

    Amefafanua kuwa,wataendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa namna yoyote ile na yupo tayari kumtetea Rais na kamwe hatakubali kuona jina la mama linachezewa na mtu yoyote.

    Aidha amesema kuwa, wanachotakiwa kutambua wao ni kuwa,kama kura zimetosha au hazijatosha warejee kujenga chama cha mapinduzi ,huku akiwataka kutoa ushirikiano wa kutosha kukisapoti chama .

    Kwa upande wake Katibu wa ccm mkoa wa Arusha,Musa Matoroka amesema kuwa,wao kama jumuiya ya wazazi wanatakiwa kutafuta kura za ccm katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na uchaguzi wa dola ifikapo 2025.

    Naye Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Arusha, Hezron Mbise amesema kuwa,jumuiya hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa nyuki ambayo imeleta manufaa makubwa sana .

    Mwisho.

    Post Views: 93
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleAMANI GULUGWA ASHINDA TUZO YA WAKURUGENZI BORA
    Next Article TAKUKURU ARUSHA WAANZA UCHUNGUZI FEDHA ZA BODA BODA ZILIZO PIGWA MILION 400 MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.