Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»IKUNGI WALIPWA FIDIA NA JESHI MILIONI 243.7

    IKUNGI WALIPWA FIDIA NA JESHI MILIONI 243.7

    0
    By arushatv on November 10, 2022 Break News

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa vijiji vya choda na mkiwa wilaya ya Ikungi.

    Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ta Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amesema Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi 112 wa kijiji cha mkiwa na wananchi 48 wa kijiji cha Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia.

    Kwa upande wao baadhi ya wananchi ndugu Mayunga Mayunga luhende na Pascal Michael Ghula pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kuwalipa fidia ili wapishe shughuli za kambi ya jeshi katika kata ya mkiwa wamepongeza mchakato wote wa uthamini kuwa wa wazi na wa ukweli.

    Katika hatua ingine Mhe. Muro pia aliwaomba viongozi wa jeshi wanaosimamia kambi ya mkiwa kutumia busara kwa kuwaruhusu wananchi wamalize kutoa mazao yao ambayo waliyapanda katika mashamba yanayozunguka kambi hiyo kutokana na wao kuandaa na kupanda kabla ya kulipwa fidia ombi lililokubaliwa na msimamizi wa kambi hiyo.

    Mwisho .

    Post Views: 83
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTAIFA LIKO SALAMA YANGA YAWATUPA WAARABU YATINGA MAKUNDI MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article WALIOSHIKWA MKONO NA NABII MKUU GEOR DAVIE WAMSHUKURU WAMO VIONGOZI WA SERIKALI

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.