Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Elimu»DKT ,MPANGO AWATAKA WAITIMU WA VYUO VIKUU KULETA MABADILIKO KATIKA TAIFA USUSANI MATUMIZI YA TEHAMA

    DKT ,MPANGO AWATAKA WAITIMU WA VYUO VIKUU KULETA MABADILIKO KATIKA TAIFA USUSANI MATUMIZI YA TEHAMA

    0
    By arushatv on November 25, 2022 Elimu

    Mwanza

    Wahitimu wa Vyuo Vikuu wameaswa kutumia vema elimu wanayopata kuleta tija kwa Taifa.

    Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Mhe. Dkt. Phillip Mpango wakati wa mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

    Aidha, Mhe. Mpango ameagiza Wizara ya Elimu kuhakikisha vituo vyote vya Chuo hicho vinaunganishwa na mkongo wa Taifa ili kuwezesha matumizi ya TEHAMA na kupunguza gharama za uendeshaji .

    “Vituo vyote vya Chuo Kikuu Huria vitaunganishwa na mkongo wa Taifa na hili naagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha linafanyika mara moja ili kupunguza gharama za uendeshaji,” ameongeza Mhe. Mpango.

    Awali akiongea katika mahafali hayo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Chuo Kikuu Huria kimetengewa fedha kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, kusomesha wahadhiri na miradi mingine.

    “Serikali kwa kutambua mchango wa Chuo Kikuu Huria katika kupeleka elimu kwa jamii kupitia mradi wa HEET tutajenga maabara saba katika mikoa ya Njombe, Arusha, Dodoma, Mwanza, Kigoma, Mtwara na Pwani ambazo zitajikita katika tafiti za kisayansi kulingana na shughuli na mahitaji muhimu ya eneo husika,” amefafanua Waziri Mkenda.

    Waziri Mkenda ameongeza kuwa Serikali imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kujenga vituo vya Chuo Kikuu Huria katika mikoa ya Geita, Kigoma, Lindi, Simiyu na Manyara ambao mikoa hii ilikuwa ikitumia majengo ya kukodi kwa gharama kubwa.

    Zaidi ya Wahitimu 4,000 wametunukiwa Shahada mbalimbali zikiwemo Shahada Umahiri na Uzamivu wakiwemo wanafunzi kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ghana, Malawi, Zambia, Congo, Namibia na Ethiopia.

    Post Views: 64
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRAIS SAMIA AWAPA UJUMBE MAWAKILI WA EAC EPUKENI RUSHWA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article MAKAA YA MAWE YATAJWA KUPANDA BEI MARA DUFU KUTOKANA NA VITA VYA UKRAINE NA URUSI

    Related Posts

    SHULE YA BILIONEA SANINIU LAIZER YAPATA UFADHILI MZITO WA MADAWATI NA MEZA ZA KISASA

    March 13, 2023

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri.mkubwa

    February 28, 2023

    WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI WALIO FUTIWA MATOKEO YA MITHIANI WA KIDATO CHA NNE

    February 9, 2023

    WANAFUNZI 170 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KUTOKA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI.

    January 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.