Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»BODI YA WAHANDISI (ERB)YAJIPANGA KUPAMBANA NA RUSHWA NA KUKUZA WELEDI

    BODI YA WAHANDISI (ERB)YAJIPANGA KUPAMBANA NA RUSHWA NA KUKUZA WELEDI

    0
    By arushatv on November 10, 2022 Habari

    Na Doreen Aloyce, Dodoma.

    KATIKA kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini,Bodi ya wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi wa sekta ikiwemo na kupambana na vitendo vya rushwa.

    Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya wahandisi Bernad Kavishe amesema Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili.

    “Wahandisi pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na maslah yetu binafsi nyuma na ndio maana tunachukua kiapo kuapa kuweka maslahi ya Umma mbele,

    ” Bodi ipo mstari wa mbele katika kupambana na rushwa manake rushwa ni adui wa uhai siyo tu adui wa haki lakini malengo mahususi ya bodi ni kuimarisha na kuhakikisha udhibiti wa kazi za wahandisi na taaluma ya wahandisi kwasababu uhandisi hauishii shuleni uhandisi ni tunahakikisha mpaka mtu ana staafu” amesema Mhandisi Kavishe.

    Aidha Mhandisi Kavishe ametoa wito kwa watu wenye miradi kuacha kutumia wahandisi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ili kuondokana na malalamiko pale wanapoharibiwa kazi zao.

    “Kinyume cha sheria kabisa kupata huduma za kihandisi nje na watu ambao hawajadhibitishwa na bodi mbalimbali za kitaaluma, ile leseni tunayokabidhi ile ndio kielelezo ambacho serikali imeipitisha kwamba huyu mtu kapata elimu sahihi hawana mashaka nae na ujuzi wake upo hai”amesema Mhandisi Kavishe.

    Nae Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara majengo na tayari imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na endapo miradi ikiharibiwa ERB inahusika.

    “Kuna kazi kubwa inafanyika na miradi mingi ndani ya nchi yetu ambayo inategemea ushauri wa wahandisi hawa na nichukue nafasi hii kuwapongeza mpaka sasa nchi yetu imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na 26 wapo sokoni wanafanya kazi, ikumbukwe kuwa tulipokuwa tunapata uhuru mwaka 1961 tulikua na wahandisi wawili tuu leo tunazungumzia hawa walio kazini na vijana bado wapo vyuoni wanasoma wanaendelea kuzalishwa” amesema Msigwa

    Mwishoo

    Post Views: 89
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWALIOSHIKWA MKONO NA NABII MKUU GEOR DAVIE WAMSHUKURU WAMO VIONGOZI WA SERIKALI
    Next Article TAWA YASHIRIKI VIVUTIO VYA UTALII NYANDA ZA JUU KUSINI.

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.