Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATANGAZA NEEMA KWA VIWANDA VIKUBWA NCHINI

    WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATANGAZA NEEMA KWA VIWANDA VIKUBWA NCHINI

    0
    By arushatv on October 11, 2022 Habari

    Na Mwadishi wa A24Tv

    Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt Ashatu Kijaji ( Mb.) amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha viwanda vya nguo nchini vinavyoajiri watu wengi hususani wanawake na vijana vinafanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza ajira, pato la taifa, kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi na uchumi kwa ujumla.

    Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha nguo cha A TO Z Bw. Kalpesh Shah akiwa na Meneja Mauzo ya Nje wa Kiwanda hicho Bw. Sylvester Kazi Oktoba 10, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadili na kitatua changamoto zinazoikabili sekta ya nguo nchini.

    Aidha, katika kuendeleza sekta hiyo, Dkt. Kijaji amesema Serikaki inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi ili kuhakikisha pamba inayozalishwa nchini inakuwa na ubora unaotakiwa na inatosheleza mahitaji ya viwanda vya nguo nchini kwa mwaka mzima ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.

    Dkt. Kijaji pia amesema ni muhimu kuanzisha viwanda vya kuchakata pamba (Spinning) nchini ili kuongeza thamani katika zao la pamba na kupunguza uuzaji wa pamba ghafi ambayo asilimia 70 ya pamba inayozalishwa nchini huuzwa nje ya nchi kama malighafi.

    Post Views: 82
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSERIKALI YATOA VIVUTIO VYA UWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA VYA DAWA
    Next Article Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe Wilaya ya Njombe wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara .

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.