Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe Wilaya ya Njombe wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara .

    Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe Wilaya ya Njombe wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara .

    0
    By arushatv on October 11, 2022 Habari

    Na Emmanuel octavian

    Katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Njombe baadhi ya wakazi hao akiwemo Peter Kyamani na Lucy Mligo Wamesema ubovu wa barabara hasa wakati wa masika umekuwa ukikatisha mawasiliano pamoja na mazao kuozea shambani.

    Awali diwani wa kata ya Lupembe Michael Mbanga amesema changamoto ya miundombinu ya barabara ni kubwa hususani katika kipindi cha masika kwani shughuli za kiuchumi zimekuwa zikisimama.

    Mtaalam wa ujenzi toka Wakala wa barabara za mijini na vijjini TARURA wilaya ya Njombe Mhandisi Mussa Mwansule amekiri kuwapo kwa changamoto ya miundombinu hiyo huku akisema itatazamwa katika bajeti ya mwaka ujao kwani kwa sasa hakuna bajeti.

    Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema ni muhimu TARURA wakaona namna ya kwenda kufanya marekebisho hata kwenye maeneo korofi badala ya kuacha kabisa barabara kusubiri mwaka wa fedha ujao huku akiwataka watumishi kuwasikiliza madiwani wanapowafuata kuwaeleza kero mbalimbali.

    Mkuu wa wilaya ya Njombe katika ziara yake ametembelea na kufanya mikutano katika kijiji cha Igombola kata ya Lupembe pamoja na vijiji vya Madeke na Mfiriga kata ya Mfiriga

    Post Views: 67
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATANGAZA NEEMA KWA VIWANDA VIKUBWA NCHINI
    Next Article TUME YA MADINI YAENDELEA KUIPAISHA SEKTA YA MADINI

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.