Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»RAIS SAMIA KESHO ,KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ARUSHA .

    RAIS SAMIA KESHO ,KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ARUSHA .

    0
    By arushatv on October 4, 2022 Break News

    Na Geofrey Stephen Arusha

    Rais ,Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano wa 65 wa kimataifa wa shirika la utalii duniani(UNWTO) unaotarajiwa kufanyika kesho Oktoba 5,2022 katika hotel ya kitalii ya Grand  Melia ,jijini Arusha.

    Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha,Waziri wa maliasili na utalii,Balozi Dkt.Pindi Chana alisema mkutano huo utahudhuriwa na Katibu mkuu wa shirika la UNWTO,Zurab Pololikashvili.
    “Pia utano huu unatarajia kukutanisha mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka nchi wananchama wa UNWTO wa kanda zaidi ya 50 kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la Uviko 19,”alisema Balizi Dkt.Chana.
    Alisema Uviko 19 umeathiri utalii wa kimataifa kwa wastani wa kati ya asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania .
    Dkt.Chana alisema mkutano huo utakuwa chachu ya kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda,watoa huduma kwenye mnyororo wa utalii,wawekezaji pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.
    katika mkutano huo pia patafanyika matukio mbalimbali ambayo ni pamoja na jukwaa la uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini ambapo pia itazinduliwa Investment Guideline(Tourism Doing Business) sambamba na  Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu masuala ya masoko.
    ” Pia kutafanyika uzinduzi wa A tour ofa African Gastronomy  pamoja na ziara za mafunzo(FAM Trips) ambapo watapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania  ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro,Jumuiya ya wanyama pori ya Buruge na city Tour ya vivutio mbalimbali katika jiji la kitalii la Arusha,”alisema.
    Waziri Chana alisema kulingana na sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za serikali katika kuongeza idadi ya watalii nchini pamoja na kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii kimkakati hususani utalii wa mikutano.
    Alisema kuwa mkutano huo utawezesha kujengea uwezo wataalam wao na wadau wa utalii katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini, Kulingana na shabaha yao ya kuongeza idadi  ya watalii milioni tano na mapato ya dola za marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.
    “Mkutano huu ni fursa adhimu ya kukuza uchumi wa jiji la Arusha ,mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla hivyo anatoa rai kwa wananchi katika kuchangamkia  fursa zitakazotokana na mkutano huu,”alisema .
     
    Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella  amesema Mkutano huo utakuwa na  fursa adhimu ya kukuza uchumi wa jiji la Arusha ,mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla hivyo anatoa rai kwa wananchi na wakazi wa Arusha  katika kuchangamkia  fursa zitakazotokana na mkutano huo.
    Mwisho .
    Post Views: 85
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNAIBU KATIBU MKUU WA UWEKEZAJI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA
    Next Article WIZARA YA TAMISEMI MFUPA MGUMU ULIO WASHINDA MAWAZIRI ! MAGAZETI YA LEO NA A24TV

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.