Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»NAIBU KATIBU MKUU WA UWEKEZAJI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    NAIBU KATIBU MKUU WA UWEKEZAJI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    0
    By arushatv on October 4, 2022 Makala

    Na Mwadishi wa A24Tv Geita .

    Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ally Gugu amefanya ziara kwenye Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Ukanda wa Uwekezaji (EPZ) Bombambili, mkoani Geita.

    Mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Madini na Tume ya Madini na kuongeza kuwa Wizara yake ipo tayari kushirikiana na Wizara ya Madini na Taasisi zake kwenye eneo la uwekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wengi wanawekeza kwenye Sekta ya Madini.

    “Sisi kama Wizara inayoshughulikia uwekezaji tupo tayari kuendelea kuvutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini hasa kwenye eneo la madini ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali za madini huku uchumi ukiendelea kukua,” amesema Gugu.

    Maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu ya “Madini ni Fursa za Uchumi, Ajira kwa Maendeleo Endelevu”, yamejumuisha pia washiriki kutoka mataifa mbalimbali kutoka Afrika ikiwa ni pamoja na Zambia, Uganda na Burundi.

    Post Views: 64
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBiteko Afungua Mkutano wa Jumuiya ya Wajiolojia Nchini
    Next Article RAIS SAMIA KESHO ,KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ARUSHA .

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.