Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»RAIS SAMIA ASHAURIWA KUKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI NCHINI.

    RAIS SAMIA ASHAURIWA KUKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI NCHINI.

    0
    By arushatv on October 13, 2022 Break News

    Moses Mashalla,Arusha

    Mfanyabiashara wa madini ya vito ambaye aliwahi kutajwa kuwa bilionea wa madini aina ya Spinner,Salim Alaudin maarufu kama “Salim Almasi” amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kukutana na wafanyabiashara wa sekta ya madini nchini ili waweze kumweleza changamoto wanazopitia.

    Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ulanga ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake.

    Akizungumza na waandishi wa habari Mfanyabiashara huyo amesema kwamba Rais Samia ni vyema akaitisha kikao na wadau wa sekta ya madini nchini kama ambavyo anakutana na makundi mbalimbali ndani ya jamii.

    “Rais Samia ni vyema akutane na wadau wa sekta ya madini ili tuweze kumshauri na kumweleza masuala mbalimbali kama changamoto tunazopitia “amesema Alaudin.

    Hatahivyo,amesema kwamba serikali ina wajibu wa kuweka mazingira rafiki hususani katika usafirishaji wa madini mbalimbali nje ya nchi kwa kuwa wamekuwa wakikumbana na vikwazo mbalimbali.

    Hatahivyo,Mfanyabiashara huyo amesema kwamba ana matarajio ya kuanzisha utalii wa madini katika eneo lake la mgodi wilayani Mahenge kama njia mojawapo ya kuwavutia watalii nchini.

    Mfanyabiashara huyo amesema kwamba katika eneo hilo tayari amejenga nyumba ya kifahari kwa ajili ya watu kufikia ambapo wageni mbalimbali watapata fursa ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanyika mgodini hapo jambo ambalo litachangia kukuza sekta ya utalii nchini.

    Amesisitiza kuwa anatarajia kununua usafiri wa ndege aina ya helicopter ambayo itarahisisha usafiri kwa watu wanaotembelea eneo hilo ambapo pia wanafunzi wa shule mbalimbali watapata fursa ya kujifunza shughuli za uchimbaji zinazoendelea katika eneo hilo.

    “Matarajio yangu makubwa ni kuona watanzania wanavaa madini yao wenyewe hata kama kwa gharama ndogo na sio wageni pekee “amesema Mfanyabiashara huyo.

    Mwisho

    Post Views: 120
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticlePROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI
    Next Article MIAKA 23 BILA BABA WA TAIFA HII NDIO HISTORIA YAKE MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.