Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»BILIONI 4 TOKA MILTENBURG UJERUMANI KUBORESHA MAZINGIRA MJI WA NJOMBE

    BILIONI 4 TOKA MILTENBURG UJERUMANI KUBORESHA MAZINGIRA MJI WA NJOMBE

    0
    By arushatv on October 2, 2022 Habari

    Na Emmanuel octavian

    Halmashauri ya mji wa Njombe inatarajia kutekeleza mradi wa kuboresha mazingira wa Takribani shilingi bilioni 4 kwa mashirikiano na mji wa Miltenburg wa nchini Ujerumani katika miradi miwili ya awali kwa awamu tofauti ikiwemo kubadili taka kuwa rasilimali pamoja na uzalishaji umeme wa jua na kuupeleka kwenye gridi ya taifa.

    Hoja hiyo imewasilishwa katika mkutano maalum wa baraza la madiwani la kujadili ufungaji wa hesabu za mwaka wa fedha uliopita ambapo wageni toka nchini Ujerumani wamefika kujifunza namna ya kwenda kutekeleza mradi huo kwa pande zote mbili ambapo nao watakwenda kutekeleza watakayojifunzi katika halmashauri ya mji ikiwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Erasto Mpete akisema kutakuwa na manufaa makubwa katika kuboresha mazingira.

    Sebastian Rundig ni Meneja mazingira katika mji wa Milternburg ujerumani ambaye amesema wanatarajia kujifunza masuala mbalimbali ya mazingira pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya umeme wa sola utakaokwenda kuchangia kwenye gridi ya taifa.

    Mkuu wa wilaya ya Njombe kissagwakisakasongwa amesema mwezi oktoba wanatarajia kwenda nchini ujerumani kuwasilisha andiko hilo ili waweze kupata fedha hizo huku mwandishi wa mradi huo Emmanuel George ambaye ni katibu tawala wilaya ya Njombe akisema mahusiano mema baina ya halmashauri ya mji wa Njombe na Milternburg ndiyo yamesababisha kuendelea vyema na mradi huo.

    Baadhi ya madiwani akiwemo Nestory Mahenge na Tumain Mtewa wamesema endapo mradi huo utafanikiwa basi itakuwa ni fursa kubwa kwa wananchi katika kuboresha mazingira. Kauli mbiu ya kuundea na kuutekeleza mradi huo ni”kuuweka mji katika hali ya kijani na safi.

    Post Views: 97
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNABII GEORDAVIE APONGEZWA KWA MISAADA ANAYO MWAGA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article DKT. BITEKO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI NA TAASISI ZAKE KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.