Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Wananchi Monduli waomba uzio kulinda vyanzo vya maji.

    Wananchi Monduli waomba uzio kulinda vyanzo vya maji.

    0
    By arushatv on September 15, 2022 Habari, Magazeti

    Mwandishi wetu, Monduli

    AWananchi wa Kata ya Selela na Engaruka wilayani Monduli mkoa Arusha,wameomba serikali kuwasaidia kuweka uzio katika vyanzo vya maji vya asili katika maeneo yao ili visiendelee kuharibiwa na wanyamapori.

    Kata hizo zina vyanzo vya maji vya asili ambazo zimekuwa zikitoa maji kwa mwaka mzima ambayo ndio tegemeo kwa mahitaji ya Maji katika Kata hizo kwa matumizi ya majumbani,kilimo na mifugo

    Wakizungumza na waandishi wa habari za Mazingira,kupitia mradi wa Utunzwaji Mazingira kwa maarifa asilia unaendeshwa na taasisi ya wanahabari ya MAIPAC na taasisi ya CILAO mradi ,anaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia program ya miradi midogo na kuratibiwa na taasisi ya jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) walisema kama vyanzo hivi havitakwa uzio vitaharibika.

    Halima Mollel alisema wanyamapori hasa Tembo wamekuwa wakivamia vyanzo hivyo na kuleta madhara jambo ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuwekewa uzio.

    “Sisi kama jamii tunavitunza vyanzo hivi kwa maarifa yetu ya asili Sasa tunaomba na serikali kutuunga mkono”alisema

    Awali Afisa Misitu wa tarafa ya Makuyuni na Manyara, Happiness Masaki alisema Wananchi wa Selela na Engaruka wametunza vyanzo ya Maji kwa maarifa ya asili na Sasa wananufaika.

    Masaki alisema Kata hizo kwa Sasa Zina maji mwaka mzima licha ya maeneo mengine kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

    “Sisi kama serikali tunawapongeza Hawa Wananchi kwa kutumza hivi vyanzo kutokana na kujiwekea sheria ndogondogo za kimila ambazo zimekuwa rafiki kwa vyanzo vya maji na Mazingira”alisema

    Katibu wa Kamati ya Mazingira Kata ya Selala,Isack Diagwa alisema Siri ya mafanikio ni kushirikisha jamii katika.utunzwaji vyanzo vya maji.

    “Lichaya ya kuwa na sheria za serikali kutunza maji pia tunatumia maarifa ya asili ambapo kila mwananchi anawajibika kutunza vyanzo hivi ikiwepo kutoingiza mifugo kwenye vyanzo,kutokana mti ama kulima”alisema.

    Mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa asilia unatekelezwa na taasisi ya wanahabari ya Usaidizi wa jamii za Pembezoni (MAIPAC) na shirika la msaada ya kisheria la CILAO na kuratibiwa na jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF).

    Mwisho.

    Post Views: 190
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAUWAJI YATIKISA , MWALIMU AUA MKE KISA WIVU ,MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article Mtakwimu mkuu asema sensa imeingiza Tanzania kwenye rekodi za kidunia

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    SIMBA YANGA YATINGA ROBO FAINALI KWA KISHINDO ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    March 20, 2023

    MAJALIWA AWASHIA MOTO WAKUU WA WILAYA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    March 19, 2023

    PANGA LASAMIA LAPITIA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    March 17, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.