Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»Viongozi wa mila wasaini makubaliano kukubali mradi wa bomba la mafuta

    Viongozi wa mila wasaini makubaliano kukubali mradi wa bomba la mafuta

    0
    By arushatv on September 16, 2022 Makala

    mwandishi wetu,.Arusha

    Viongozi wa mila wa Masai,Barbeig,Akie na wataturu wamesaini makubaliano ya kukubali kushiriki katika mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga.

    Viongozi hao wamesaini makubaliano na uKampuni ya ujenzi wa boma la mafuta ya EACOP Tanzania hafla iliyofanyika Mountmeru hoteli na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanyakazi na jamii hizo.

    Akizungumza kwa niaba ya wazee wa mila ,Laigwanani Joseph Laizer amesema wamekubali kuwa na makubaliano na kampuno ya EACOP baada ya kuwashirikisha katika mradi huo.

    “sisi kama viongozi tumeridhishwa na makubaliano ya leo na tutakwenda kuwa mabalozi kwa wengine”amesema

    Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka kampuni ya EACOP kutekeleza yote walioyokubamiana.

    Mkurugenzi wa kampuni ya EACOP Tanzania, Wendy Brown amesema watatekeleza yote waliyoahidi.

    “tutashirikiana katika mpango kazi wa mradi wa bomba la mafuta na tutahakikisha mnanufaika”amesema.

    Amesema watawashirikisha katika utekelezaji wa mradi, kuzijengea uwezo jamii hizo katika masuala ya kiuchumi,kuzisaidia kupata huduma muhimu kama elimu na afya, kuendeleza masuala tamaduni.

    Afisa Nishati kutoka wizara ya Nishati, Yovin Uisso amesema serikali itahakikisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya EACOP na jamii hizo yatatekelezwa na pande zote.

    Amesema katika kuhakikisha jamii hizo zinanufaika na mradi huo serikali itatoa fursa ya upendeleo kwa baadhi ya vitu ikiwepo ajira.

    Mshauri elekezi wa mradi huo, katika masuala ya haki za binaadamu, Dk Elifuraha Laltaika, amesema kampuni EACOP imesaini makubaliano na jamii hizo ikiwa ni kuheshimu sheria na vigezo vya kimataifa zinazolinda haki za jamii za pembezoni.

    Amesema masuala yq haki za jamii hizo yamezingatiwa katika mradi huo.

    viongozi waliosaini makubaliano hayo ni kutoka wilaya za Simanjiro,Kiteto,Kilindi,Handeni,Igunga,Kondoa na Hanang.

    MWISHO.

    Post Views: 55
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRC NJOMBE APIGA MARUFUKU WATOA MIKOPO UMIZA KUWARUBUNI WALIMU SHULENI
    Next Article MAJI YA MAITI YAIBUA TAHARUKI KUOSHEA SAMAKI,MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV.

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.