Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Vijiji 20 Longido vyatenga hekta 186.794 kwa ajili ya nyanda za malisho

    Vijiji 20 Longido vyatenga hekta 186.794 kwa ajili ya nyanda za malisho

    0
    By arushatv on September 19, 2022 Habari

    Mwandishi wetu,

    Arusha. Vijiji 20 kati ya 49 wilayani Longido, mkoa wa Arusha, vimetenga eneo la hekta 186.794.2 kwa ajili ya nyanda za malisho ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

    Katika wilaya hii, asilimia 95 ya wakazi ni wafugaji ambao wanamiliki mifugo 918,248 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 hata hivyo hivi sasa wamekosa malisho ya mifugo na maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

    Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Longido, Nestory Daqarro akizungumza na waandishi wa habari za mazingira kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa maarifa asilia ambao unafadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia programu ya miradi midogo alisema wilaya hiyo, imeathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi.

    Daqarro alisema kutokana na uhaba wa malisho ya mifugo na maji katika wilaya hiyo, hivi sasa wafugaji wamehamia maeneo ya nje ya wilaya hiyo kusaka malisho hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo wameamua kutenga maeneo ya nyanda za malisho ambapo watapanda majani na kuweka maji.

    “serikali inatambua changamoto za wilaya kwani kwa mwaka wa pili sasa hakuna mvua za kutosha hivyo, vijiji vimetenga maeneo ya nyanda za malisho ambayo yataidhinishwa na serikali kuu ili kuokoa mifugo yao”alisema

    Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kimokowa wilaya ya Longido,Kilel Olenyokie Mollel alisema wameamua kutenga maeneo ya nyanda za Malisho ili kuyatunza kwa ajili ya ufugaji.

    “Tumekuwa tukikabiliwa na Ukame katika wilaya yetu hivyo tumeona ni vizuri kutenga maeneo ya malisho ambayo hayatavamiwa”alisema

    Mwenyekiti Kijiji Cha Olbomba Kashira Alais alisema wamekuwa wakitumia maarifa ya asili katika uhifadhi hata hivyo wanataka serikali kutambua maarifa hayo ili kupunguza migogoro.

    Masono ole Malendai alisema wanawake wamekuwa waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi lakini wanaamini suluhu ni matumizi ya maarifa asilia.

    Mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa asilia unatekelezwa na shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni la MAIPAC kwa kishirikiana na CILAO na unataratibiwa na Jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF).

    Mwisho

    Post Views: 62
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWaziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji amewataka wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha 21th Century kil Kufanya kazi kwa Saa 24 Tutatatua changamoto
    Next Article POLISI NJOMBE WAKIRI KUNA SHIDA YA MIGOGORO

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.