Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»VIJANA WAPATIWA MAFUNZO NA SIDO KUJIKWAMUA KATIKA AJIRA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO

    VIJANA WAPATIWA MAFUNZO NA SIDO KUJIKWAMUA KATIKA AJIRA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO

    0
    By arushatv on September 9, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen Arusha .

    Katika kuakikisha vijana wanajikwamua katika ajira kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la viwanda vidogo SIDO,kupitia mradi wa wanagenzi , imewawezesha vijana wapatao 130 mkoani Arusha ,kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia viwanda vidogo ,ambayo yamewasaidia kuwapatia ujuzi na uthubutu katika sekta hiyo.

    Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Rasilimali watu Mkoani hapa,David Lyamongi wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa vijana hap 130 waliohitimu mafunzo ya viwandani  pamoja na kuwatunuku vyeti wanagenzi, iliyofanyika jijini Arusha.

    Lyamongi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela,alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanatumia uzoefu walioupa kubuni na kwenda kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowasaida kujiajiri na kupunguza janga la ajira hapa nchini. 

    Katibu tawala huyo alilipongeza shirika la SIDO kwa kutekeleza vema mradi huo unaosimamiwa na serikali kupitia wizara ya  Elimu,Sayansi na Teknolojia na  kufadhiliwa na benki ya dunia ambapo alisema ,serikali inatambua changamoto za vijana.

    Awali meneja wa SIDO mkoa wa Arusha,Jafary Donge aliishukuru serikali kwa kukubali kuwapatia mafunzo na mitaji vijana hao ambayo yamesaidia kuwapatia uzoefu mahala pa kazi.

    Alisema hadi sasa mradi huo umefanyika katika mikoa 12 na kuwafikia vijana 1647nchini huku mkoa wa Arusha kupitia halmashauri ya Arusha DC,Meru na jiji ukiandikisha vijana  130 wakiwemo wanawake 66.

    Alisema kuwa jukumu la SIDO  katika mradi huo ilikuwa ni kuratibu vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao walihitimu mafunzo ya SIDO na katika taasisi na vyuo mbalimbali.

    “Baada ya kuwapata vijana hao tuliwaunganisha na wanagenzi ambao waliwapatia mafunzo katika viwanda vyao kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikiwapatia kiasi cha sh.100,000 kila wiki kama fedha ya kujikimu “alisema.

    Alisema vijana hao  walishiriki na kufuzu  mafunzo ya uokoji wa mikate,usindikaji wa vyakula,asali na Vipodozi,Utengenezaji wa Sabuni,Ushonaji,Uhandisi, ufundi magari , utalii na Urembo.

    Baadhi ya wanagenzi,Ally Babu kutoka kampuni ya uokaji mikate ya Bilsarm ,Irene Baker na Ahmed Abdalah (Dallerz Group)waliipongeza serikali kwa hatua ya kuwapatia mafunzo vijana kupitia viwanda ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na wimbi la ajira hapa nchini.

    “Mpango huu ni mzuri kwani unatusaidia hata sisi kupata wafanyakazi bora tuliowafundisha wenyewe na pia utasaidia kupunguza wimbi la ajira kwa baadhi yao watakaojiajiri “alisema Irene Manzi anayemiliki  Irene Baker  eneo la Majengo na Maromboso jijini hapa.

    Ends…

    Post Views: 49
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTOZO KAA LA MOTO YATIKISA VIKAO VYA CCM ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article MWENYEKITI MPYA WA TLP HUYU HAPA NI MKONGWE WA SIASA TLP ITAFIKA MBALI

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.