Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Siasa»MWENYEKITI MPYA WA TLP HUYU HAPA NI MKONGWE WA SIASA TLP ITAFIKA MBALI

    MWENYEKITI MPYA WA TLP HUYU HAPA NI MKONGWE WA SIASA TLP ITAFIKA MBALI

    0
    By arushatv on September 9, 2022 Siasa
    Na Mwandishi wa A24Tv Dar es Saalam
    mrithipiic

    Sekretarieti ya Chama cha TLP kimemchagua Hamad Mkadam kurithi kwa muda nafasi  ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Augustine Mrema.

    Mrema alifariki Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa akipatiwa matibabu.

    Uchaguzi huo umefanyika leo Ijumaa Septemba 9, 2022 katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, Hamad Mkadamu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Zanzibar ameshinda kwa kura nne dhidi ya  mpinzani wake Dominata Rwechungura (Bara) aliyepata kura mbili kati ya kura sita zilizopigwa na wajumbe sita.

    Akizungumza leo, Ijumaa Septemba 9, 2022 Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo baada ya kutangaza matokeo hayo amempongeza Hamad, amesema atakuwa anafanya kazi za mwenyekiti wa chama hicho hadi utakapoitwa mkutano mkuu wa kuchagua Mwenyekiti wa Taifa.

    ” Uchaguzi wetu ulikuwa na wagombea wawili ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Upande wa Zanzibar na Bara, Hamad ameshinda kwa kupata kura nyingi zaidi tutakuwa tunamuunga mkono kuhakikisha Chama kinaendelea kupiga hatua,” amesema Richard

    Baada ya ushindi huo Hamad amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kwamba anajiona anajukumu kubwa la kuenzi mazuri yote yaliyoachwa na Hayati Mrema.

    “Chama lazima kipige hatua, pamoja na shukurani zangu kwa wajumbe wenzangu kwa kuniamini bado nina kazi ya kuenzi mazuri yote ya mtangulizi wangu kwa kipindi chote na kuongeza mengine mapya kikubwa naomba ushirikiano,” amesema

    Katika hatua nyingine Lyimo amesema Wajumbe hao wamemteua mtoto wa Mrema, Michael Mrema kuwa Mjumbe wa Sekretarieti kuu ya Chama hicho ikiwa ni kuthamini mchango alioutoa kiongozi wao huyo.

    Mwisho .

    Post Views: 287
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleVIJANA WAPATIWA MAFUNZO NA SIDO KUJIKWAMUA KATIKA AJIRA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO
    Next Article MALKIA ELIZABETH ALILIWA KILA KONA YA DUNIA ! KWA WEMA WAKE MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

    March 5, 2023

    CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

    January 17, 2023

    JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

    January 4, 2023

    MIKUTANO YA HADHARA RUKSA IGP WAPE VIBALI MUDA WOWOTE

    January 3, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.