Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»LHRC YAWASIKILIZA WATU 796 KWA SIKU KUMI

    LHRC YAWASIKILIZA WATU 796 KWA SIKU KUMI

    0
    By arushatv on September 27, 2022 Habari

    Na Emmanuel Octavian

    Njombe

    Jumla ya madai 796 ya kesi mbalimbali yameripotiwa kwa mawakili mbalimbali wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na kupatiwa msaada wa kisheria pasina malipo yoyote huku migogoro ya ardhi ikiwa kinara mkoani Njombe.

    Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na haki za binadamu Anna Henga amesema licha ya wanawake wengi kukumbwa na mikasa mbalimbali ikiwemo ya kupokwa ardhi,kukatiliwa na kunyimwa haki mbalimbali lakini idadi yao katika kuripoti madai yao imekuwa ndogo ukilinganisha na wanaume.

    Henga ametoa ripoti hiyo mkoani Njombe wakati wa kufunga maadhimisho ya miaka 27 ya kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 1995 ambapo mfumo dume ungali unaripotiwa katika jamii.

    Wananchi mkoani Njombe akiwemo Richard Mligo na Dorcas Siame ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wa sekondari wa club za haki za binadamu wanasema migogoro mingi katika jamii inachagizwa na kukosekana kwa msaada wa kisheria na gharama kubwa za kutafuta mawakili.

    Katibu mkuu wizara ya Katiba na Sheria Mery Makondo kwa niaba ya Waziri wa katiba na sheria anakiri kuwapo kwa changamoto kubwa ya kucheleweshwa kwa haki kwa wananchi na kwamba serikali imeliona suala hilo na kuanza kulifanyia kazi.

    Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga anasema wananchi wengi wanafungwa jela kwa kukosa msaada wa kisheria hivyo kituo cha sheria na haki za binadamu kiwe mkombozi kwao kupitia vituo vya msaada wa kisheria.[Paralegal].

    Kutokana na kukithiri kwa migogoro mingi ya ardhi nchini Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary anasema serikali imeanzisha ofisi za ardhi kila halmashauri ili kukabiliana na tatizo hilo.

    Mwaka 1995 kituo cha sheria na haki za binadamu kilianzishwa kikishughulikia changamoto mbalimbali za kukosekana kwa haki za binadamu zinazosababisha ukatili katika jamii.

    Post Views: 82
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MADINI NA MKUU WA WILAYA YA GEITA WATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA
    Next Article CCM YAFUTA CHAGUZI 5 VIGOGO WAANGUKIA PUA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.