Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MADINI NA MKUU WA WILAYA YA GEITA WATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MADINI NA MKUU WA WILAYA YA GEITA WATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    0
    By arushatv on September 27, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24T Geita

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo leo Septemba 27, 2022 wametembelea banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

    Mara baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalam wa Tume ya Madini, Naibu Katibu Mkuu ameitaka Tume ya Madini kuendelea kutoa elimu hasa katika eneo la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ili wananchi wengi waweze kushiriki kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini na kujipatia kipato huku Serikali ikipata mapato yake.

    ” Wananchi wengi bado wanahitaji elimu kuhusu fursa zilizopo kwenye migodi ya madini na kuanza kutoa huduma kama vile vyakula, ulinzi n.k,” amesema Mbibo

    Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo ameitaka Tume ya Madini kuendelea kutoa elimu kuhusu Sheria ya Madini ili kuzuia migogoro kati ya wananchi na wawekezaji kwenye shughuli za madini.

    “Mnafanya kazi nzuri sana lakini ni vyema mkaweka nguvu zaidi kwenye utoaji elimu kwa wawekezaji na wananchi wanaomiliki mashamba ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza wakati wa shughuli za uchimbaji wa madini,” amesema Shimo

     

    Post Views: 90
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticlePADRI ABAKA WATOTO 10 KILIMANJARO ,ASOMEWA MASHTAKA 3 MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article LHRC YAWASIKILIZA WATU 796 KWA SIKU KUMI

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.