Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»KIHAMIA AKABIDHI OFISI WAKURUGENZI WAMLILIA ALIKUA MCHESHI MSIKIVU

    KIHAMIA AKABIDHI OFISI WAKURUGENZI WAMLILIA ALIKUA MCHESHI MSIKIVU

    0
    By arushatv on August 3, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen Arusha .

     ARUSHA

    Aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Athuman Kihamia amekabidhi ofisi kwa katibu tawala mpya ,Musaa Albano Qkisisitiza kufanya kazi kwa ufanisi

    Akiwaaga watumishi wa Sekretariet ya mkoa huo dkt Kihamia alisema Kuwa amekuwepo Arusha kwa kipindi kifupi cha miezi 14 tangia ateuliwe wadhifa huo

    Akiongelea miradi mbalimbali aliyoitekeleza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 alisema mkoa ulipokea shilingi bilioni 1.3, kwa ajili ya ukarabati Jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa,ukarabati nyumba ya mkuu wa wilaya ya Arusha,sanjari na ujenzi wa ukuta wake wa uzio  ukarabati ofisi ya mkuu wa wilaya ya Longido ,uchimbaji kisima kirefu cha maji ,ofisi ya mkuu wa mkoa.

    Alisema kuwa ukarabati ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa,ujenzi ,ukarabati choo cha ofisi ya mkuu wa wilaya ukarabati wa nyumba ya Katibu tawala mkoa ukarabati nyumba ya mkuu wa mkoa, ukarabati wa ofisi mbilii za tarafa .n.k.

    KATIBU Tawala mpya wa mkoa wa Arusha,Mussa Albano ameahidi  kutekeleza  majukumu yote yaliyoachwa na watangulizi wake ,akaomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wengine wa serikali ili awaze kutekeleza ipasavyo majukumu yaliyopo.

    Aliyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika jengo la mkuu wa  mkoa,na kusisitiza ushirikiano kwa watumishi wengine wa serikali ili kutimiza majukumu yaliyopo mbele yao na. kutoa huduma bora kwa wananchi.

    Mwezi uliopita Rais Samia Suluhu Hassani,alifanya mabadiliko ya baadhi ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala,ambapo alimuondoa aliyekuwa katibu tawala mkoa wa Arusha dkt Athumani Kihamia na nafasi yake kuchukuliwa na Mussa ambae amehamia kutoka mkoa wa Songwe

    Kaimu Katibu tawala mkoa wa Arusha, Abeli Ntupa,amempongeza aliyekuwa katibu tawala wa mkoa huo  dkt Athumani Kihamia,kwa utendaji wake uliotukuka ambao umeacha alama,isiyofutika ambayo wataitumia kama mwongozo.

     

    Ntupa,ambae pia ni Katibu tawala msaidizi,elimu,Sekretariet ya mkoa,ameeleza kuwa dkt Kihamia alikuwa kiongozi mwelekezaji ,aliimarisha system ya utendaji ambayo wataendelse kuifanyia kazi kwa kuwa ina mafanikio makubwa kwrnye utumishi wa umma.

    Alisema walikuwa wakifanyia kazi maelekezo kwa haraka na sasa kasi hiyo ya uwajibikaji wataitumia kutekeleza maelekezo ya  uwajibika ya katibu tawala mpya.

    Katibu tawala msaidizi huduma za afya kwenye sekretariet ya mkoa, dkt Silvia Mamkwe,amesema kuwa dkt Kihamia  amewajengea timuwork kwa kufanyakazi kwa pamoja ,alikuwa mwelekezaji na mshauri,aliwajali watumishi wa ngazi za chini wakiwemo wenye ulemavu

    Mamkwe,ambae ni mganga mkuu wa mkoa  wa Arusha,alisema kuwa mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja umeongeza ufanisi na kuwepo ubunifu mambo ambayo yamechangia uboreshaji wa utendaji na kuongeza kuwa shughili za umma ni kupokezana vijiti

    Katibu tawala msaidizi rasilimali watu Sekretari ya mkoa, David Lyamongi,alisema kihamia alikuwa ni kiungo ,mzuri sana aliimarisha mawasiliano ya haraka kwa kasi kubwa katika halmashauri zote saba za mkoa huo hivyo watamkumbuka

    Alisema kuwa dkt,Kihamia, alissiitiza watumishi kufanya kazi kwa viwango  alisimamia na kuelekeza maswala ya utumishi ikiwemo watumishi kulipwa saa za ziada kunapokuwepo kazi za dharura

    Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Raphael Siumbu,kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri zingine  za mkoa huo, alisema kuwa dkt Kihamia alikuwa kiongozi  mwadilifu,mcheshi ,hivyo watatoa ushirikiano kwa katibu tawala mpya.

    Mwisho.

     

    Post Views: 215
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWITO WATOLEWA MATUMIZI YA LUGHA YA KUFUNDISHIA, UBORESHAJI SERA YA ELIMU
    Next Article BEI YA MAFUTA WADAU WATOA MAONI ! KUPANDA TENA MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.