Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WITO WATOLEWA MATUMIZI YA LUGHA YA KUFUNDISHIA, UBORESHAJI SERA YA ELIMU

    WITO WATOLEWA MATUMIZI YA LUGHA YA KUFUNDISHIA, UBORESHAJI SERA YA ELIMU

    0
    By arushatv on August 3, 2022 Habari

    Na WyEST,
    ZANZIBAR

    Wito umetolewa wa kufanya matayarisho ya kutosha ya matumizi ya lugha itakayokubalika kufundishia hasa kwa upande wa walimu na wanafunzi katika ngazi zote za Elimu nchini.

    Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mwanahamisi Ameir wakati akifungua kikaokazi cha maoni ya uchambuzi na tathmini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kinachofanyika Zanzibar.

    Amesema kuwa matayarisho ya walimu upande wa mafunzo ni ya muhimu katika kuhakikisha walimu wapya wanaozalishwa na ambao wapo tayari kazini wanakuwa na vigezo vinavyotakiwa.

    “Matayarisho ni ya muhimu kujua vitu kama sifa za wanaoenda kusomea ualimu, sifa za vyuo, muda wa mafunzo uweje, matayarisho ya walimu kumudu lugha husika ya kufundishia, vyote hivi vitolewe kwa kiwango katika vyuo vyote ili kupata walimu wenye sifa stahiki,” amefafanua Ameir.

    Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti wa timu ya Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Prof. Joseph Semboja amesema lengo la kikaokazi hicho ni kupokea maoni kutoka kwa wadau wa elimu kutoka upande wa Zanzibar juu ya maboresho ya Sera hiyo.

    Kikaokazi hicho kinachotarajiwa kuhitimishwa kesho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto, Abeda Rashid Abdallah na wadau mbalimbali wa Elimu kutoka Bara na Kisiwani humo.

    Post Views: 55
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMADED 85 MATATANI! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV .
    Next Article KIHAMIA AKABIDHI OFISI WAKURUGENZI WAMLILIA ALIKUA MCHESHI MSIKIVU

    Related Posts

    Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini waaswa kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa MKUMBI

    March 30, 2023

    SHIRIKA La Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia

    March 30, 2023

    Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa maendeleo ya miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo

    March 30, 2023

    KILELE CHA TUZO YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU ,APRIL 13 2023 KUFANYIKA DAR

    March 30, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.