Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WATENDAJI WA WIZARA YA HABARI,MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WAKUTANA ARUSHA KUWEKA MIPANGO YA KUTEKELEZA BAJETI

    WATENDAJI WA WIZARA YA HABARI,MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WAKUTANA ARUSHA KUWEKA MIPANGO YA KUTEKELEZA BAJETI

    0
    By arushatv on July 26, 2022 Habari

    Moses Mashalla,

    Watendaji mbalimbali wa wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari wanakutana jijini Arusha kuweka mipango ya kutekeleza bajeti ya wizara hiyo sanjari na kutathimini changamoto mbalimbali.

    Hivi karibuni bunge la jamhuri lilipitisha bajeti ya wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari jumla ya kiasi cha sh,282.05 kama matumizi ya kawaida na miradi mbalimbali ya maendeleo.

    Akizungumza katika kikao hicho naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Mathew Kundo alisema kwamba wamekutana kwa lengo la kufanya tathmini na mpango wa kutekeleza bajeti hiyo ambayo ilipitishwa Hivi karibuni na bunge la jamhuri.

    Naibu waziri huyo alisema kwamba mbali na kufanya tathmini hiyo pia wanaangalia maeneo mbalimbali ya kurekebisha katika bajeti hiyo.

    “Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha habari na mawasiliano hivyo tumekutana kupanga mipango ya kutekeleza bajeti yetu “alisema Waziri Kundo

    Hatahivyo,katibu mkuu wa wizara hiyo,Dk Jimmy Yonaz alisema kuwa mkutano uliowakutanisha ni muhimu kwa kuwa utaanisha mipango ,nia na kutoa dira njema kwa wizara hiyo.

     

    Mkurugenzi wa magazeti ya serikali (TSN) Tuma Abdallah alisema kuwa mkutano huo unatoa fursa muhimu kwa watendaji wa wizara pamoja na wadau kukutana na kubadilishana mawazo namna ya kutekeleza shughuli mbalimbali ndani ya wizara hiyo.

    Dk Abdallah alisisitiza kuwa mkutano huo pia ni muhimu kwa kuwa unatoa mwanga kwa watendaji kuzitazama changamoto mbalimbali na kusukuma maendeleo ya taasisi mbalimbali zilizoko ndani ya wizara hiyo na serikali kwa ujumla.

    Mwisho.

    Post Views: 58
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWANANCHI KATA YA KIUTU WAISHUKURU HALMASHAURI KUWAJENGEA SHULE
    Next Article VILIO NA MAJONZI WANAFUNZI WALIOFARIKI AJALI YA WATU 13! RAIS ATOA POLE MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.