Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WANANCHI KATA YA KIUTU WAISHUKURU HALMASHAURI KUWAJENGEA SHULE

    WANANCHI KATA YA KIUTU WAISHUKURU HALMASHAURI KUWAJENGEA SHULE

    0
    By arushatv on July 26, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv 

    Halmashauri ya Arusha DC inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 8 katika Shule mpya ya Sekondari ya kata ya Kiutu wilayani Arumeru.

    Akiongea Wakati Mkurugenzi na viongozi wa Halmashauri hiyo walipotembelea kukagua shule hiyo Diwani wa kata ya Kiutu Malaki Malambo amesema wanaishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za Utekelezaji wa miradi.

    Amesema kwamba fedha iliyotengwa imetumika vizuri hakuna ubadhirifu na Mkurugenzi ameahidi kuongeza fedha kwa ajili ya kumalizia kazi iliyoanzwa na wananchi ambapo Kuna Madarasa nane hayajakamilika ili January wanafunzi waanze masomo kwa kidatocha kwanza.

    Ameeleza kwamba serikali kupitia Halmashauri imejielekeza kuifanya shule hiyo kuwa na kidato. cha tano na cha kwanza ambayo itapokea hapo mwakani wanafunzi wa kidato Cha kwanza January.

    Kwa Upande Wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Selemani Msumi ameahidi kutoa fedha za umaliziaji wa shule hiyo na kusema kuwa wapo katika Mchakato wa kusubiria fedha.

    Amesema kwamba pamoja na Lengo shule hiyo imekuja wakati muafaka Halmashauri inapojiandaa na mkakati wa kuongeza vyanzo vya mapato na kumshukuru Diwani wa kata hiyo kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo

    Mkurugenzi huyo wa Halmashauri Anabainisha kwamba fedha za Mradi huo ni kiasi Cha Milion 470 ya fedha zilizotolewa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa sekondari hiyo mpya ya kata ya Kiutu ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa sekta ya Elimu.

    Airene Olais Mkazi wa Kijiji Cha Olgilai kata amesema wanaishukuru Halmashauri hiyo na viongozi kwa kuja na wazo la kuanzisha shule hiyo kwani awali kata hiyo haikuwa na shule hivyo imekuja Wakati muafaka

    Amesema kwamba shule hiyo pia itawasaidia watoto wa Jamii ya kifugaji kutotembea umbali mrefu kwenda kata za jirani kufuata shule kwani Sasa itakuwa Karibu na kata hiyo.

    Post Views: 54
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMSD, KUNANUKA RUSHWA WAZIRI AAGIZA KUFUMULIWA! MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article WATENDAJI WA WIZARA YA HABARI,MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WAKUTANA ARUSHA KUWEKA MIPANGO YA KUTEKELEZA BAJETI

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.