Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»PROF.SEDOYEKA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA NCAA NA KUHIMIZA UIMARISHAJI HUDUMA ZA UTALII

    PROF.SEDOYEKA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA NCAA NA KUHIMIZA UIMARISHAJI HUDUMA ZA UTALII

    0
    By arushatv on July 27, 2022 Habari

     

    Na Mwandishi wa A24Tv .NCAA
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Eliamani Sedoyeka tarehe 26 Julai, 2022 amefanya ziara katika ofisi za NCAA Karatu Mkoani Arusha kwa lengo la kukutana na Menejimenti kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi.

    Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa kufuatia ongezeko la wageni ni muhimu kuhakikisha kuwa mda wote mitambo inakuwepo barabarani kwa ajili ya kurekebisha sehemu korofi ili kuboresha mawasiliano ya barabara kwa wageni mda wote.

    “Kwa sasa Ngorongoro ni moja ya maeneo yanayotembelewa na wageni wengi, Utaratibu mliouanza wa kuweka mitambo ya kurekebisha sehemu korofi uendelee ili kuhakikisha barabara katika maeneo ya Hifadhi zinakuwa bora mda wote”

    Ameupongeza uongozi wa NCAA kwa jitihada za kutangaza utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

    Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt. Christopher Timbuka amemueleza katibu Mkuu kuwa mkakati wa Mamlaka ni kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi kutoka wageni 700,000 waliotembelea Hifadhi mwaka 2018/2019 kabla ya athari ya ugonjwa wa UVIKO-19 hadi kufikia idadi ya wageni 1, 200,000 ifikapo mwaka 2025.

    Post Views: 263
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAANDAMANO YA UHAMASISHAJI WA SENSA NA MAKAZI JIJINI ARUSHA NA VIONGOZI WA DINI ,MILA
    Next Article YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.