Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»DIWANI WA VITI MAALUM MBUGUNI AMTUMIA SALAMU RAIS SAMIA,AGUSIA MIKOPO YA WANAWAKE NCHINI.

    DIWANI WA VITI MAALUM MBUGUNI AMTUMIA SALAMU RAIS SAMIA,AGUSIA MIKOPO YA WANAWAKE NCHINI.

    0
    By arushatv on July 25, 2022 Habari

    Moses Mashalla,

    Diwani wa viti maalumu (CCM) kata ya Mbuguni wilayani Meru mkoani Arusha,Husna Abdallah amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa vitendo kuwa mwanamke akipewa nafasi anaweza kuitumikia kwa uweledi na kufanya vizuri tofauti na ilivyozoeleka.

    Diwani huyo alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na waandishi wa habari jijini Arusha huku akisema kuwa Rais Samia amekuwa ni alama na ameonyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kuongoza wakipewa nafasi.

    “Rais Samia amekuwa ni alama kwetu sisi wanawake na ametuoyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kuongoza wakipewa nafasi hata za juu “alisema Diwani Husna

    Alimpongeza Rais Samia kwa kumwaga fedha za ujenzi wa zahanati mbalimbali nchini ambapo katika kata ya Mbuguni ametoa jumla ya sh,50 milioni za ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ambao ulikwama tangu mwaka 2019.

    Hatahivyo,ameishauri serikali iongeze fedha za kutosha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake,vijana na walemavu kwa kuwa mwitikio umekuwa mkubwa sana.

    Serikali hutoa fedha kwa halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya kukopesha makundi mbalimbali ambapo wanawake hupewa asilimia 4,vijana asilimia 4 huku walemavu wakiambulia asilimia 2.

    Diwani huyo alisema kwamba serikali inapaswa kuweka mpango mkakati wa kuongeza fedha za kutosha kwa halmashauri mbalimbali kwa kuwa fedha zinatolewa kwa sasa hazitoshi na mwitikio wa kukopa fedha hizo umekuwa ni mkubwa.

    Diwani huyo alisema kwamba halmashauri nyingi nchini hazina mapato ya kutosha kwa kuwa zinategemea mapato ya fedha za ndani ambazo hazitoshi.

    “Serikali inapaswa kuongeza fedha za kutosha kwa halmashauri mbalimbali nchini ili ziweze kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake,vijana na walemavu kwa kuwa halmashauri nyingi zinategemea mapato ya ndani ambayo hayatoshi na ukizingatia mwitikio umekuwa ni mkubwa sana “alisema Diwani huyo

    Hatahivyo,alisisitiza kuwa wabunge na madiwani kupitia mikutano wanayoifanya wanapaswa kutoa elimu na mrejesho kwa wananchi kuhusu mikopo inayotolewa kwa lengo la kuongeza mwamko.

    Alisisitiza kuwa ni muda mwafaka sasa serikali ina wajibu wa kutengeneza programu ya kutoa elimu ya kutosha kuhusu mikopo inayotolewa na halmashauri mbalimbali nchini kwa kuwa eneo la upande wa elimu bado ipo chini.

    “Lakini pia maafisa maendeleo wa kata wawatembelee hawa wakinamama na kuzungumza nao kuhusu hii mikopo ili wapate mrejesho na kuwapa hamasa “alisisitiza Husna

    Mwisho….

    Post Views: 63
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMchungaji Nasari ashauri watoto wafundishwe maadili mema ili kukomesha mauaji nchini
    Next Article RAIS SAMIA AWAONYA BODA BODA KUTUMIKA VIBAYA MAGAZETI YA LEO NA A24TV

    Related Posts

    Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini waaswa kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa MKUMBI

    March 30, 2023

    SHIRIKA La Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia

    March 30, 2023

    Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa maendeleo ya miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo

    March 30, 2023

    KILELE CHA TUZO YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU ,APRIL 13 2023 KUFANYIKA DAR

    March 30, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.