Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Business»Mchungaji Nasari ashauri watoto wafundishwe maadili mema ili kukomesha mauaji nchini

    Mchungaji Nasari ashauri watoto wafundishwe maadili mema ili kukomesha mauaji nchini

    0
    By arushatv on July 24, 2022 Business

    Moses Mashalla,

    Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Akheri ,Anael Nasari ameshauri watoto wafundishwe uungwana na maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kukomesha janga la mauaji nchini.

    Hivi karibuni kumeripotiwa habari za mauaji ya mara kwa mara yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi.

    Akizungumza katika ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT usharika wa Akheri mchungaji Nasari alisema kwamba watoto wanapaswa kufundishwa maadili na uungwana tangu wakiwa wadogo ili wakikua wawe na tabia njema.

    “Watoto wafundishwe maadili mema tangu wakiwa wadogo ni lazima uungwana uanzie katika ngazi ya familia “alisema Mchungaji Nasari

    Hatahivyo,alisema kuwa matukio ya mauaji yanayoendelea nchini yanaakisi jamii iliyovurugwa na isiyostaarabika na kuitaka serikali ichukue hatua.

    Mchungaji Nasari alisema kuwa ni lazima jamii ifuate ibada na malezi bora na kuondokana na ndoa za kubahatisha zisizofuata taratibu za mila,desturi na taratibu.

    “Ndoa za kubahatisha hazifai tumekosa malezi ni lazima sasa tuheshimu mila,taratibu na sheria za ndoa lakini tuzingatie ibada “alisisitiza Mchungaji Nassari.

    Mchungaji Nassari alimalizia kwa kuwataka walimu,wazazi,wanasiasa na jamii kwa ujumla kuacha kutumia lugha za matusi na kejeli ili kuepuka kujenga kizazi cha watoto wasio na maadili na heshima mbele ya jamii.

    Mwisho…

    Post Views: 86
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNYONGEZA YA MSHAHARA PASUA KICHWA! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article DIWANI WA VITI MAALUM MBUGUNI AMTUMIA SALAMU RAIS SAMIA,AGUSIA MIKOPO YA WANAWAKE NCHINI.

    Related Posts

    WAZIRI MKENDA AZINDUA MKOPO WA ELIMU KUTOKA BENK YA NMB.

    March 15, 2023

    Tanzania na China Kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara

    February 27, 2023

    RC MAKALA AISHUKURU BENKI YA NMB KUZAMINIA ZIARA YA VIONGOZI MACHINGA NA BODABODA RWANDA.

    February 4, 2023

    BANK YA UBA YAFIKA ARUSHA WAFANYA BIASHARA WAFURAIYA RIBA NAFUU

    January 20, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.