Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»KAZI INAENDELEA YA UTATUZI WA MIGOGORO – IKUNGI

    KAZI INAENDELEA YA UTATUZI WA MIGOGORO – IKUNGI

    0
    By arushatv on June 14, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv 

    Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro pamoja na wataalam kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri wameendelea na ziara ya utatuzi wa kero za wananchi na safari hii wamefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Choda kata ya Mkiwa jimbo la singida mashariki

    Dc Muro pamoja na wataalamu walilazimika kwanza kufanya mkutano wa ndani na halmashauri ya kijiji cha choda pamoja na kamati ya usimamizi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na kukubaliana kuwasilisha mpango huo kwenye mkutano wa kijiji siku hiyo hiyo hatua iliyomaliza mgogoro na mvutano wa muda mrefu

    Kutatuliwa kwa mgogoro huo kumetoa nafasi kwa mwekezaji kutoka Jordan kuanza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 12 katika wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa kutengeneza mafuta ya alizeti, pamoja na kuanza kilimo cha alizeti ambacho kitamuwezesha pia kuzalisha mbegu za alizeti kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi katika eneo lenye hekari 1,700 katika kijiji cha choda

    Dc Muro amewaomba wananchi kuufuata na kuutekeleza kwa dhati mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kijiji cha choda mpango ambao utaondoa na kumaliza migogoro yote ya ardhi katika eneo hilo

    Post Views: 95
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWaandishi wa habari na Wahariri wa Mitandao ya Kijamii katika mafunzo ya Sensa 2022
    Next Article Waziri Mwigulu tozo ya miamala kupungua

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.