Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»MENEJA WA MGODI WA GEM $ ROCK AENDELEA KUSOTA POLISI YEYE NA WENZAKE 21 KUPANDISHWA MAHAKAMNI MUDA WOWOTE KWA KUVAMIA MGODI WA KITALU C

    MENEJA WA MGODI WA GEM $ ROCK AENDELEA KUSOTA POLISI YEYE NA WENZAKE 21 KUPANDISHWA MAHAKAMNI MUDA WOWOTE KWA KUVAMIA MGODI WA KITALU C

    0
    By arushatv on March 15, 2023 Habari

    Na John Mhala,Mirerani

    Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture,Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti ametiwa mbaroni na wenzake 21 na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa tuhuma za kuongoza genge la Wachimbaji wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wana Apollo na kuvamia kinyemela ndani ya mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Kitalu C katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro.

    Mgodi wa Kitalu C unaochimbwa kwa ubia kati ya Serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise ulivamiwa marchi 12 mwaka huu majira ya kati ya saa 6.30 na saa 8 mchana na kundi hilo wakiwa na silaha za jadi na majabali makubwa yenye ncha kali na kufanikiwa kuwajeruhi zaidi ya wafanyakazi 10 wa kampuni ya Franone ambao hali zao bado ni mahututi na wako katika hospital ya rufaa ya KCMC ya Mjini Moshi Mkoani Kilimanjro.

    Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara,Kamishina Msaidizi,George Katabazi alisema kuwa polisi imefanikiwa kumkamata Saitoti ambaye inadaiwa kuwa ndio kiongozi Mkuu wa uvamizi huo na bado anahojiwa katika kituo Kikuu cha Polisi Mirerani.

    Katabazi alisema mbali ya Saitoti kuna wana Apollo wengine wamekamatwa ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Gem & Rock Venture,kampuni inayomiki mgodi wa Tanzanite ulipo kitalu B mpakani wa mgodi wa Kitalu C unaochimbwa na kampuni ya Franone unaomilikiwa na Mbise.

    Kampuni ya Gem & Rock Venture unaomiliki Mgodi wa Tanzanite uliopo Kitalu B unamilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wauzaji na Wanunuzi wakubwa wa Madini ya Tanzanite Tanzania{TAMIDA}.

    Alisema kama taratibu za upelelezi na mahojiano zikikamilika huenda wakafikishwa Mahakamani mapema kujibu mashitaka lakini ikishindikana basi watafikishwa mahakani kesho.

    ‘’Tumemkamata Saitoti ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Gem & Rock Venture na pia ndio aliyekuwa kiongozi wa kuongoza genge la wavamizi katika mgodi wa serikali na mbia mwenza’’alisema Katabazi

    Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone unachimba mgodi wa kitalu C alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kusema juu ya tukio hilo na kusema kuwa ameiachia polisi kushughulika na wavamizi hao wenye ni ovu kwake.

    Mwisho

    Post Views: 57
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI MKENDA AZINDUA MKOPO WA ELIMU KUTOKA BENK YA NMB.
    Next Article NI AIBU ZITTO KABWE APOKELEWA NA MADUMU !AWESO AELEZEA CHANGAMOTO YA MAJI .MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.