Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Kundi kubwa la watalii wapatao 17 kutoka nchini Ufaransa watembelea mgodi Kitalu C wa kampuni ya Franone Mining

    Kundi kubwa la watalii wapatao 17 kutoka nchini Ufaransa watembelea mgodi Kitalu C wa kampuni ya Franone Mining

    0
    By arushatv on March 13, 2023 Habari
    Na Geofrey Stephen Manyara
    Kundi kubwa la watalii wapatao 17 kutoka nchini Ufaransa wametembelea mgodi wa kuzalisha madini aina ya Tanzanite katika mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na  kampuni ya Franone Mining iliyopo  wilayani Simanjiro Mkoani Manyara .
    Vitus Ndakize akitoa maelezo kwa wageni walio fika kitalu c kuanvalia namna ya uzalishaji wa madini ya Tanzanite yanavyo zalishwa
    Kundi hilo ambalo  ndani yake wapo wataalamu wa kukata na kuongeza thamani ya madini pamoja na wanafunzi wa kuongeza thamani ya madini  wamesema wamefurahia kuona sehemu pekee inayochimbwa madini ya Tanzanite mkoani Manyara.
    Kundi la watalii kutoka nchini Ufaransa wakisikiliza kwa makini namna uzalishani wa madini ya Tanzanite yanavyo zalishwa katika mgodi wa kisasa wa kitalu C unaomilikiwa na kampuni ya mzawa wa Franone Maning 
    Akizungumza  mara baada ya kupokea kundi hilo, Meneja mkuu wa kampuni ya Franone Mining , Vitus  Ndakize  amesema wamejisikia faraja kubwa kwa wageni hao kufika katika mgodi pekee  mkubwa yanapo patikana madini aina ya Tanzanite .
    “Kitendo cha hawa watalii kufika kwenye mgodi  wetu kimekuwa  ni faraja kubwa sana kwani tumeweza kujifunza mengi pia kutoka kwao na tumeweza kuweka historia  kwa kutembelewa  na kundi hili  ambalo wameweza kujionea namna ya utendaji  kazi wetu.”amesema .
    Ndakize ameshukuru wizara ya madini kwa kuwakaribisha watalii hao wa sekta ya madini kwani ujio wa wageni hao unaendelea kutangaza nchi ya Tanzania kwamba madini ya Tanzanite yanapatikana pekee nchini Tanzania na sio pengine.
    Aidha ameongeza kuwa, kwa sasa mgodi huo umeshaanza kazi rasmi na wanategemea uzalishaji mkubwa kutokana na wataalamu wa miamba  kutoka  maeneo ambayo madini yanapatikana  licha ya mgodi huo kutokufanya kazi kwa muda wa miaka mitano .
    ‘Serikali ilitangaza tenda mwaka 2022 mwezi wa wa nne  ambapo kampuni ya Franone Mining ilishinda tenda hiyo mwezi wa sita na kupewa leseni ya uchimbaji mwezi wa saba mwishoni  huku serikali ikiwa na ubia  asilimia 16 na mpaka sasa umeanza kazi za uchimbaji ikitegemea kuanza uzalishaji wa madini ya Tanzanite  wakati wowote “amesema Meneja .
    Kwa upande wake Mmoja wa watalii ,  Camille Constant kutoka nchini Ufaransa amesema amepata uzoefu wa kipekee wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite hivyo atakua balozi mzuri kwa wenzake pamoja na watalii wengine .
    “Nimefurahishwa  sana na namna ya  uchimbaji wa kisasa ambao unatumika kuchimba na  kupata madini ya Tanzanite ikilinganishwa na maeneo mengine walio tembelea katika nchi za Africa kusini , Ivory Cost na Ufaransa kwani nimeona   utofauti mkubwa sana katika uchimbaji na nimepata uzoefu wa kutosha pia.”amesema Camille.
    Mwisho.
    Post Views: 63
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRUSHWA YA NGONO BADO TATIZO NCHINI , MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article TASAC YaAKANUSA TAARIFA ZINAZO ZAGAA MITNDAONI NI KUHUSU KUVUNJiWA MIKATABS n KABLA.

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.