Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    0
    By arushatv on March 16, 2023 Habari

    Na Geofrey Stephen Arusha .

    Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni 2.22_

    Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa leo tarehe 16 Machi, 2023 amezindua rasmi mfumo wa ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) na wa utoaji wa huduma kwenye jamii unaofanywa na migodi ya madini (CSR)

    Dkt. Kiruswa amefanya uzinduzi huo kwenye Jukwaa la Pili la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini linaloendelea jijini Arusha linalokutanisha kampuni za uchimbaji wa madini, watoa huduma wa madini kwenye migodi ya madini na Taasisi za Kifedha.

    Akizungumzia mfumo huo, Naibu Waziri Kiruswa amesema kuwa mfumo utawezesha kampuni za uchimbaji wa madini na watoa huduma kwenye migodi ya madini kuwasilisha nyaraka mbalimbali kwenye uwasilishaji wa mipango ya ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na utoaji wa huduma kwa jamii kwenye migodi ya madini kwa njia ya kieletroniki badala ya kutumia nakala ngumu kama ilivyokuwa ikifanyika awali.

    Ameongeza kuwa, mfumo pia utarahisisha zoezi la uchakataji wa maombi yanayowasilishwa Tume ya Madini na majibu ya maombi kutolewa kwa wakati na watalaam kutoka Tume ya Madini.

    Katika hatua nyingine, akielezea mafanikio ya maboresho ya Sheria ya Madini yaliyopelekea kutungwa kwa kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa ni pamoja na mabadiliko makubwa kufanyika ikiwa ni pamoja na kuchochea ongezeko la fursa mbalimbali katika nafasi za ajira na mafunzo, uhaulishaji wa teknolojia, utafiti na maendeleo, matumizi ya huduma na bidhaa zinazotolewa na kuzalishwa na watanzania.

    Amefafanua kuwa ajira kwa watanzania katika migodi mikubwa zimeongezeka kutoka 6,668 mwaka 2018 hadi kufikia 15,341 mwaka 2022 pamoja na watanzania wanaopata mafunzo mbalimbali ya kujengewa uwezo wa kufanya kazi ambazo baadhi zilikuwa zinafanywa na wageni ambapo katika kipindi cha mwaka 2022, jumla ya watanzania 8,066 walipatiwa mafunzo mbalimbali katika Sekta ya Madini na kujengewa uwezo katika utendaji kazi ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.4 zilitumika.

    Naibu Waziri Kiruswa ameendelea kueleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ongezeko la manunuzi ya ndani ya nchi ambapo mwaka 2022 jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 2.22 sawa na asilimia 97.4 ya manunuzi yote ya kampuni za madini yalifanyika kwa kutumia kampuni za watanzania, ukilinganisha na Dola za Kimarekani milioni 238.71 sawa na asilimia 46 ya manunuzi yote kwa mwaka 2018 kutumika.

    Ameongeza kuwa, kumekuwepo na ongezeko la watoa huduma kwenye migodi ya madini ambapo kwa mwaka 2022 wamefikia 1386 sawa na asilimia 81 ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo kulikuwa na watoa huduma 623.

    Naye Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo ameongeza kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini bado inaendelea kutoa elimu katika mikoa mbalimbali nchini kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini ili wananchi wengi waweze kushiriki kwenye shughuli za utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.

    Mwisho .

    Post Views: 28
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNI AIBU ZITTO KABWE APOKELEWA NA MADUMU !AWESO AELEZEA CHANGAMOTO YA MAJI .MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.