Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Naibu waziri uwekezaji na Viwanda Kigahe tumieni teknologia kwa mabadiliko ya tabia ya Nchi

    Naibu waziri uwekezaji na Viwanda Kigahe tumieni teknologia kwa mabadiliko ya tabia ya Nchi

    0
    By arushatv on December 5, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen . Arusha

    Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe amewataka wawekezaji wanaoshindana katika sekta ya viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki ili kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa inayochangia mabadiliko hasi ya tabia nchi.

    Hayo yalisemwa jana Jijini Arusha na Naibu Waziri Kihage wakati wa ufunguzi wa kongamano la madhimisho ya Ushindani Duniani katika kilele cha siku ya ushindani Duniani.

    Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe Akifungua Mkutano huo 

    Alisema endapo endapo kampuni hizo zitazingatia matumizi sahihi ya matumizi ya hewa ukaa itasaidia kupunguza hewa ukaa inayochangia mabadiliko ya tabia nchi.

    Alisema lengo la wafanyabiashara wote ni kupata faida hivyo lazima kuhakikisha ushindani wa haki unazingatiwa ikiwemo kuhakikisha mamlaka ya ushindani zinazuia ukiritimba katika biashara ikiwemo nguvu ya soko kuwameza washindani katika biashara.

    Pia kudhibiti muingiliano wa biashara katika unaolenga kuwaweza washindani katika baadhi ya biashara na kuongeza kuwa ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi unahatarisha usalama na uhatarishi wa theluji katika mlima Kilimanjaro.

    “Wawekezaji katika sekta ya Viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki katika kudhibiti mazingira ikiwemo wanyama katika sekta ya utalii katika upunguzaji wa ikolojia ya wanyama ikiwemo ukataji ovyo wa miti ikiwemo mkaa ”

    Alitoa rai kwa wadau mbalimbali kupanda miti ili kudhibiti uongezeko la hewa ukaa hivyo ni lazima miti ipandwe katika kulinda ikolojia ya wanyama sanjari na uoto asili

    Naye Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC),Dk,Aggrey Mlimuka Alisema kongamano hilo ni muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na uendelevu na ushindani katika kuhakikisha utalii unakua kwa kasi sanjari na ulinzi wa mazingira

    Alisema kauli mbiu ya mwakahuu ni ushindani na maendeleo endelevu kwani kuwepo kwa Utalii huo endelevu kunahitaji juhudi za pamoja katika kulinda mazingira ikiwemo ufanyaji biashara na kuleta ushindani.

    Huku Jaji Salma Maghimbi kutoka Baraza la Ushindani alitoa rai kwa mawakili kuhakikisha wanazingatia kanuni na sheria katika uendeshaji wa kesi za ushindani katika kuhakikisha kesi zinasikilizwa na kutolewa maamuzi.

    Awali Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Injinia Richard Ruyango alitoa rai kwa wadau mbalimbali katika sekta ya mazingira kuhakikisha mazingira yanalindwa ili kuzuia chagamoto za mabadiliko ya tabia nchi na ikolojia.

    Mwisho

    Post Views: 91
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleHABARI KUBWA ! MABEHEWA,22 YENYE KEMIKALI YAANGUKA MOROGORO MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article HABARI KUBWA , SHEREHE ZA UHURU ZAFUTWA MILION 960 KUJENGA MABWENI YA WENYE ULEMAVU ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.