Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»MBUNGE GAMBO KUTISHIWA MAISHA KUTAKA KUUAWA, NDIO NASIKIA ARUSHA IKO SALAMA

    MBUNGE GAMBO KUTISHIWA MAISHA KUTAKA KUUAWA, NDIO NASIKIA ARUSHA IKO SALAMA

    0
    By arushatv on December 13, 2022 Break News
    Na Mwandishi wa A24Tv . Arusha 

    Dc Mtanda amjibu Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kutoa madai ya kutishiwa kuuawa na watu aliodai ni viongozi  wa serikali,

    Mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi  Mtanda kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kufika ofisini kwake kueleza kwa kina madai ayo 

    “Kama Mbunge  alitishiwa maisha kwanini hakutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ,kama unatuhuma yoyote unatakiwa wewe mwenye ukathibitishe kwenye vyombo vya usalama”

    Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mtanda alidai kutokuwa na taarifa za mbunge huyo kutaka kuuawa akisisitiza kuwa taarifa hizo hana na wilaya ya Arusha ipo salama .
    Hata hivyo Mtanda alimshangaa Gambo ambaye amepakana naye kiofisi , kutompa taarifa hizo nzito akidai hata Dodoma walikuwa pamoja lakini hakumwambia chochote badala yake taarifa hizo anazisikia kupitia vyombo vya habari.
    Siku chache zilizopita Gambo akihutubia mkutano wa hadhara eneo la soko kuu jijini hapa,alitamka pasipo kupepesa macho kuwa ,amevamiwa mara mbili nyumbani kwake na kuna watu wanamwinda wamuue na baadhi yao anawafahamu ni viongozi wa serikali.
    Mbunge Gambo alisema watu hao wamekuwa wakimwinda ili wamuue  kwa sumu lakini wameshindwa kwa sababu yeye sio mtu wa kula ovyo ovyo labda wamvamie getini wampige risasi ,tuhuma ambazo ni nzito.
    Mwisho
    Post Views: 399
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI PINDI CHANA TAFUTENI VYANZO VIPYA VYA MAPATO KUKUZA UTALII NCHINI
    Next Article HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO ,MAMA NA MWANAE MBARONI KWA MAUAJI YA BABA YAO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.