Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Makilayoni FC bingwa wa Chemchem CUP 2022

    Makilayoni FC bingwa wa Chemchem CUP 2022

    0
    By arushatv on December 7, 2022 Habari

    Mwandishi wetu, Babati

    Timu ya soka ya Makilayoni FC juzi imetwaa ubingwa wa michuano ya Chem chem CUF 2022 baada ya kuichabanga timu ya Mdori FC kwa penati 4-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Mdori wilayani Babati,mkoa Manyara.

    Katika mchezo huo, ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa Manyara, Makongoro Nyerere hadi dakika 90 zilipomalizika timu hizo zilitoka zimefungana 1-1.

    Baada ya ushindi huo mabingwa hao ambao wametwaa mara mbili mfululizo mwaka2021 na 2022 wakipewa zawadi ya fedha taslim sh 1 milioni kombe lenye thamani ya sh 1 milioni na Mpira.

    Katika michuano hiyo ambayo mwaka huu lengo lilikiwa ni kupiga vita ujangili wa Twiga jumla ya timu 16 zilishiriki kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Burunge(JUHIBU).

    Mdori FC wakipewa zawadi ya Kombe na fedha taslim 500,000,Mpira ambapo awali timi zote 16 zilipewa seti ya jezi na mpira ili kushiriki michuano hiyo ikiwepo timi za mpira wa Pete..

    Akizungumza katika michuano hiyo,Mkuu wa mkoa Manyara Makongoro Nyerere aliwataka vijana kushiriki katika kupambana na ujangili na kutunza Mazingira.

    “Michezo hii sio tu ni fursa ya kukuza vipaji na kupata burudani lakini inalenga vijana kupambana na ujangili lakini pia kuhifadhi Mazingira”alisema.

    Meneja mahusiano wa taasisi ya Chemchem, Charles Sylvester ambayo imewekeza shughuli za Utalii wa picha na hoteli katika eneo hilo la JUHIBU alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa miaka 10 iliyopita imekuwa na faida kubwa.

    “Tumepata vipaji kuna wachezaji wametoka hapa wameenda ligi kuu lakini pia vijana wengi wamekuwa malinzi wa Wanyamapori na kupenda uhifadhi na tutaendelea kuiboresha”alisema

    Mwenyekiti wa michuano hiyo, Belela Erasto alisema michuano ya mwaka huu imegharimu zaidi ya million 50 alipongeza wawekezaji ya Chemchem kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo kila mwaka.

    Erasto alisema hao waliowekeza hoteli za kitalii na Kitalu Cha Uwindaji kupitia kampuni tangu za EBN na kufanya Utalii wa picha wamekuwa na manufaa makubwa katika wilaya ya Babati na mkoa mzima wa Manyara ikiwepo kutoa ajira zaidi ya 300 ,ujenzi wa shule,kusaidia sekta ya afya,maji na vikundi vya wanawake

    Mwisho

    Post Views: 89
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI KIJAJI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WAINDONESIA, KUBORESHA USHIRIKIANO WA BIASHARA
    Next Article Tume ya sayansi na teknolojia yapongeza vyuo  kwa kuanzisha programu maalumuya mafunzo ya ujasiriamali. 

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.